Kocha wa muda wa Manchester United Ryan Giggs (kushoto) aliyechukua mikoba ya David Moyes (kulia) aliyetimuliwa leo kwa kuchemsha anawatafuta ubaya mahasimu wao Liverpool kwa kauli yake ya  kuropoka aliyoitoa mwaka 2011 na kuibuliwa leo kuwa japo  wao wako katika kipindi kigumu kimchezo lakini kamwe hawatoporomoka na kuadhirika kama iliyokuwa kwa Liverpool baada ya kunyang'anywa ubingwa na kuanza kufanya vibaya miaka 24 iliyopita.
Giggs amenukuliwa akisema kuwa japo Man U walisubiri miaka 26 kabla ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza kwa mara ya kwanza mwaka 1993, kocha wao mstaafu Ferguson ameikiimarisha kikosi chake vyema kiasi ya kwamba hakitodorora vibaya kama Liverpool.

Mashabiki wa Liverpool wameipokea kwa hamaki habari hiyo na kumtaka aombe radhi haraka sana.
"Hana adabu huyu...He must apologise. FA must demand he clarifies or apologise for bringing the game into disrepute...Mwana----" ameng'aka Mshabiki mmoja wa Bwawa la Maini,  na ambaye ni mwanachama wa umoja wa mashabiki wa Liverpool nchini Tanzania unaokwenda kwa jina la The Kop in Tanzania.
Mwanachamwa mwingine wa The Kop in Tanzania amesema: "Nimefuatilia sana hii habari, mana'ke ameniudhi sana, kumbe alisema in 2011 siku moja kabla Man U haijacheza nasi (walishinda 1-0), sasa naweza kucheka kwa sababu miaka mitatu baadaye wako mahali ambako hawakutegemea kuwa...lol! Link hii: hapa http://www.mirrorfootball.co.uk/news/Ryan-Giggs-taunts-Liverpool-by-saying-Manchester-United-could-never-collapse-like-the-Mersey-Reds-article666407.html.
"Hata kama (alisema miaka hiyo) sisi huyu bwana tunaye tu. Na Jumapili kwenye kombe la FA nyumbani kwake Old Trafford tunammalizia hasira na yeye afungashiwe virago", alisema shabiki mwingine.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...