Mashindano ya 16 ya Mpira wa Kikapu kwa Majiji ya Afrika Kanda ya Tano na Majiji alikwa kutoka Kanda zingine za Afrika yanatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mashindano yatafanyika:- Mwezi wa Mei, Tarehe 6 hadi 11 Mwaka 2014. 
 Majiji yanayotarajiwa kushiriki ni Dar es Salaam (wenyeji), Mwanza, Mbeya, Arusha na Tanga kutoka Tanzania. Nairobi, Mombasa na Kisumu kutoka Kenya. Kampala na Mukomo kutoka Uganda. 
Majiji mengine ni  Bujumbura – Burundi na Kigali-Rwanda. Mogadishu na Hargeisa kutoka Somalia. Juba na Citizen kutoka Sudani ya Kusini. Addis Ababa – Ethiopia na Cairo-Misri. Mashindano ya 15 ya Majiji yalifanyika mwezi May mwaka jana (2013) jijini Kampala; ambapo Jiji la Mukono nchini Uganda lilitwaa ubingwa kwa wanaume na Nairobi walitwaa ubingwa kwa wanawake. 
 Ni matarajio ya Kamati ya uendeshaji ya Majiji (Intercity Coordinating Committee) na Bodi ya Intercity, kwamba Majiji yote matano ya Tanzania yatakuwa yanajiandaa vyema ili kushiriki na kuhakikisha kuwa ubingwa unabakia Tanzania. 
 Tunatoa wito kwa utawala wa Jiji la Dar es Salaam kushirikiana na uongozi wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam ili kuitumia fursa hii kulitangaza Jiji na kuwapatia wafanya biashara nafasi ya kuongeza uchumi wao. 
Pia Halmashauri zote tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni kushiriki katika kuziandaa timu za wanawake na wanaume za Jiji la Dar es Salaam kwa kiwango cha kutwaa ubingwa. 
 Ingefaa nafasi ya kwanza ya udhamini ichukuliwe na Jiji pamoja na Halmashauri zake tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni na kwa pamoja kuwaalika wafanyabiashara wa Jiji la Dar es Salaam kuwaunga mkono ili shindano liwe zuri na lenye mafanikio makubwa. 
 Tunatoa wito kwa Utawala wa Majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga kusaidia maandalizi ya timu zao kwa kushiriki moja kwa moja na kwa kushawishi wadhamini wengine kudhamini timu za majiji yao. Imetolewa na kamati ya uendeshaji ya Majiji ya Africa Kanda ya Tano, Mchezo wa Mpira wa Kikiapu. 
 Mbaga Mwamboma Katibu, 
Bodi ya wakurugenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...