Mtoto Samir mkazi wa mtaa wa Langoni kata ya Miembeni,akiwa amefungwa kamba katika mguu wake wa kushoto huku upande mwingine ukiwa umefungwa katika chuma kizito kilichopo jirani na mlango.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MTOTO Samir anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne hadi mitano mkazi wa mtaa wa Langoni katika manispaa ya Moshi,amejikuta katika wakati mgumu kutokana na tabia ya bibi yake kumfunga kamba katika mguu wake kwa lengo la kumzuia asiende kucheza mbali na nyumbani kwao.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika eneo hilo ambapo bibi huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja alikutwa akiwa amemfunga kamba ya kudu mjukuu wake huyo katika mguu wa kushoto huku sehemu nyingine ikiwa imefungwa katika chuma kizito.

Kwa mujibu wa majirani walisema bibi huyo amekuwa akimfunga mtoto huyo mara kwa mara kwa zaidi ya nusu saa hasa nyakati ambazo bibi huyo amekuwa akifanya shughuli zake za usafi wa ndani pamoja na kufua.

Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina,majirani hao wamesema imekuwa ni kawaida kwa bibi huyo ambaye anaishi na wajukuu zake kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo huku akimzuia kucheza na wenzake wa nyumba za jirani.

“Sisi hiyo hali mbona tumeizoea mara kwa mara Samir akienda kucheza na wenzake huko mtaani,bibi yake akimkuta huko anamkamata na kisha kumfunga kwenye hilo chuma lililoko hapo mlangoni kwa zaidi hata ya nusu saa”alisema mmoja wa majirani.

Akizungumza tukio hilo Bibi huyo ambaye anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 60 alikiri kumfunga mtotot huyo kwa madai kuwa amekuwa mtundu kupita kiasi na kwamba ametumia mbinu hiyo ili kumdhibiti asitoroke nyumbani.

“Hapa nyumbani naishi na wajukuu zangu ,wengine wako mashuleni na wengine wako kazini ambao ni wazazi wa huyu Samir,mmoja anafanya kazi Arusha,mwingine yuko hapo mjini(Moshi)sasa sina mtu wa kunisadia kumwangalia huyu mtoto”alisema Bibi huyo.

Alisema analazimika kumfunga kamba mtoto Samir kutokana na kuwa na tabia ya kwenda kuzurura katika nyumba za watu huku wakati mwingine huenda kucheza mbali na nyumbani jambo ambalo humpa shida kumpata kwa urahisi.

“Wakati mwingine nashikwa na hasira kumpiga siwezi hivyo naamua kumfunga kamba hapa mlangoni…watu wote si wazuri kumruhusu kuingia kila nyumba huko atafundishwa mambo mabaya ndio sababu nafanya hivi.”alisema Bibi huyo.

Mmoja wa wazazi walioshuhudia tukio hilo walisema wazazi wengi wamekuwa wakikosea kuwaacha watoto wao walelewe na bibi zao hali inayochangia kuwepo kwa vitendo vya ukiukaji wa hali ya watoto na kibinadamu kama ilivyotokea kwa mtoto huyo.

“Wazazi tumekuwa bize sana na shughuli za utafutaji ,hali hii inapelekea majukumu ya kulea watoto kuiacha kwa wasichana wa kazi na hata mama zetu kama ilivyo kwa familia hii ,sasa suala hili pia wakati mwingine linachangia makuzi mabovu kwa watoto”alisema Juma Nzota.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. mbona mimi naona sawa tu kwa huyu bibi kumfunga kamba mjukuu wake ni kweli inaonekana kama anamnyanyasa ukiangalia hiyo kamba kafunga lakini kwa maelezo ya bibi sioni kama anamnyanyasa mtoto akizurura ovyoo kucheza majumbani mwa watu huenda kweli akafundishwa mambo mabaya kwa duni hii tulionayo watu wengi hawana maadili mema au kujali watoto wa wenzao kila mtu anaona mtoto wake ndo mali


    na kama anateswa mbona wazazi wa huyu mtoto wako na wanaishi na huyu bibi so iweje leo nyinyi wadaku wamagazeti mnaojidai mnahuruma naye sana mzushiye sheshe huyu bibi

    hajakosema kabisa huyu bibi kumfunga kamba huyu mjuku wake wengi tu tumelelewa na bibi zetu na tena tumelelewa vema na kukuwa na maadili mema kuliko ambavyo walio lelewa na wazazi wao si siri chunguzeni mtaona hili

    ReplyDelete
    Replies
    1. lakini naye bibi asikae mbali maana likitokea janga hapo mtoto ataathirika

      Delete
  2. Huyo Bibi hana jinsi, that is typically crying for help on her side. Shame to those parents alive and able but like to leave their kids for someone else to raise them on their behalf. Shame to those parents whose mothers cared and raised them until they became adults, and furthermore still want that favor extended to their kids. Your parents are growing older, for god's sake, instead of caring for them at old age, you want them running after your children?... totally unacceptable. Kwa Maelezo yake huyo Bibi ni bora tu alivyofanya kulikoni amwachie huyo mjukuu katika dunia hii iliyojaa Watu wa kila aina incl pedophiles.

    ReplyDelete
  3. Mimi naomba Blogu ya Jamii kwa niaba ya sisi watanzania wengine ambao tuna mapenzi mema na watoto wote bila kubagua, tunaomba mumfikishe bibi huyu kwenye vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake. na TUNAOMBA TAARIFA YA KITAKACHOJIRI.

    JAmbo hili limetutia huzuni sana, maana hata sisi sote tulikuwa watoto akiweo huyo bibi na hatukufungwa Kamba, Samir ana makosa gani kama mtoto mpaka afungwe Kamba?

    Ankal, Serious sisi tulioko mbali na nyumbani huko tuwakilishe kwenye hili na utupe Mrejesho.

    Asante na tuendeleza Libeneke.

    ReplyDelete
  4. Mi nafikiri kosa kubwa na lawama zielekezwe kwa wazazi wa huyo mtoto, wanamuachia mama yao kumuangalia mtoto mdogo,bila hata kumtafutia binti wa kazi wa kumsaidia, hawazingatii umri wake ulivyo mkubwa, hataweza kukimbia kumtafuta mtoto huko na huko kila siku. Huyu bibi seriously amekuwa worried, dunia sasa hivi imejaa watu wabaya sana, kitoto kinaweza kutekwa huko kiliko wakakifanyia unyama wowote ule licha tu ya kujifunza tabia mbaya kwa majirani. Ingawaje kitendo cha kumfunga hakikubaliki, lakini inawezekana sana huyu bibi alishapeleka kilio chake kwa wanae kuhusu huyo mtoto, lakini wanae wakapuuza, wanajua yeye si yuko tu home, hivyo hawaoni sababu ya kuingia garama; hawaoni taabu anayopata; angekuwa na umri kwenye 40-50 labda; lakini above 50 ni mtu mzima sana, si vyema kumpelekesha kwa kumuachia mtoto mtundu bila msaidizi kijana

    ReplyDelete
  5. Asee ktendo cha bibi huyu nakipinga waziwazi jambo alofanya si jema hata angalikua ni mama yangu amemfanyia hivi mwanangu daah sintofurahi....
    haitakiwi watt kulelewa na bibi zaidi jamani nikumchosha mamaako manake akili yake nayo inakua ishachoka hawez mikikii yakukimbizana na wajukuu....
    wote wana makosa kwa mzazi na bibi wamemdhalilisha mtoto mbaya....manake hapo ikitokea ajali ya moto mtt anadhurika moja kwa moja bila jitihada za uokozi.

    ReplyDelete
  6. Astakafirullah hii dunia haina huruma

    ReplyDelete
  7. Kumhukumu huyu bibi ni makosa maana inaweza kuwa hata hao wanawe wameshindikana na ndio maana bado wako nyumbani. Nadhani bibi angejua mahali pa kulilia shida zake asingeweza kumfunga kamba mjukuu wake. Msaidieni ili hao wazazi wa mtoto wawajibike na mtoto wao na si kumpa kazi ya kulea katika umri huo na kama hamna namna ya wao kama wazazi kukaa na huyo mtoto may be wako shule then wawajibike kwa kumsaidia bibi hizo shughuli nyingine ile yeye aweze kumuangalia mjukuu wake kwa karibu.

    ReplyDelete
  8. Msimuhukumu huyu bib bila kujua huyo mtoto ana tabia gani,inawezekana huyo bibi ana shughuli za kufanya za muhimu na kamfunga hapo karibu nae asikimbie kwenda nje, kama ni hivyo anakosa gani, tusijifanye tunajua haki za biniadamu wakati sisi wanaume watu wazima tunawachukua wanawake kama biniadamu daraja la pili tunawapiga na kuwanyanyasa.

    ReplyDelete
  9. Huyu Bibi hana makosa...watoto wa siku hizi ni watundu sana. Hivi mnaona ni vema mkasikia huyu mtoto ameanguka mtaroni au amelishwa sumu huko mitaani au ameumia vibaya au kupotea ndo mshangae? Watoto wanahitaji uangalizi wa karibu sana ambao huyu Bibi hawezi 24 hours. Na anamfunga only 30 minutes...mwacheni bibi wa watu anaangalia maslahi ya mjukuu wake. hawezi mbeba mgongoni...
    Solution ni kutafuta dada wa kazi ambapo ni gharama pia. Huyo mtoto akikua ataacha...pole bibi kwa malezi

    ReplyDelete
  10. Huyu bibi hana makosa hata kidogo, watoto wengine ni watundu sana na bibi hawezi kukimbizana nao. Wazazi wa huyo mtoto wanafanya nini kumwachia bibi wa watu mtoto mdogo waje kumchukua. Pengine wanaponda raha tu mjini wakati bibi anateseka na kajukuu. Safi sana BIBI.

    ReplyDelete
  11. Hongera bibi. Sijaona kosa lako. Watu wanajidai wanajua sana haki za binadamu lakini nia ya bibi ni njema sana. Mbona huko kwenye international airports tunaona kina baba kwa kina mama wamefunga watoto wao kamba mikononi ili wasipotee na hatuwakaripii? Mimi mwanangu pia mtundu na angependa sana kwenda nje kucheza na wenzie lakini kwa sababu za kiusalama huwa simruhusu. Namruhusu siku nina muda wa kumfatilia. Kwa hiyo huwa nafunga geti kwa kofuli ili asijetoroka. Nyumba ya bibi ingekuwa na geti angefanya hivyo pia. Nyie wenzetu huko ughaibuni kwa kumsaidia bibi nendeni mkajenge dei kea pale kijijini. Pia kuwalaumu wazazi wa huyo mtoto bila kujua sababu za kumuacha mtoto kwa bibi ni kujisumbua bure.

    ReplyDelete
  12. Jamani tembeeni muone.Mbona ulaya utaona mama kamfunga mwanae kamba ya mkono anatembea na kando ya barabara ili asigongwe na gari au asimtoroke.Na hizo kamba zinauzwa madukani kwa ajili hio?Mwacheni bibi wa watu kwani bado sio kosa.

    ReplyDelete
  13. Watoto wengi wanakufa kwa kutumbukia kwenye visima vya maji machafu na mashimo ya choo yasiyozibwa..funga kamba bibi ili ukimfungulia unajua nyendo zake..safi bibi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...