Ndugu zanguni, 
 Tunapenda kuwapa habari njema watu wote kuwa kuanzia tarehe 01/05/2014 Kampuni yetu inayomilikiwa na Watanzania waishio UK, inahamishia ofisi zake ndani ya bandari kubwa kuliko zote za kusafirisha magari UK , PORT OF TILBURY. 
 Sisi tutakuwa weusi wa kwanza kabisa kupewa ofisi ndani ya hii bandari na hivyo majina yetu kuingia kwenye historia. Na serikali imetukubali baada ya kuona jinsi tulivyoweza kujibeba kutoka kwenye kiosk mpaka tulipo.
 Mkumbuke Serengeti ilianzishwa kwa mtaji wa £1,800 tu. Tumepewa mkataba wa miaka 10 na tunaweza ku-renew baada ya hapo kama bado tutakuwa tunataka kuendelea na biashara ndani ya bandari Tumechukua Yard yenye ukubwa wa ekari mbili na ofisi yenye ukubwa wa 2,500sq ft. 
 Hii itatusaidia kuboresha huduma zetu kwa sababu tuna mpango wa kukodi meli ya saizi ya kati ili magari yetu yote na makontena tuwe tunasafirisha wenyewe na pia kusafirisha magari na makontena ya makampuni mengine pia. 
 Pia usalama wa mali za wateja ni maximum kwa sababu kuna zaidi ya camera 5,000, kituo cha polisi ni hatua mia tatu tu kutoka kwetu, police patrol ni 27/7 Yard /ofisi zetu zitakuwa OPPOSITE BERTH 31, BESIDE HYUNDAI TERMINAL 
 Tukiishakamilisha mkataba wa kukodi meli tutatoa punguzo kubwa kwa usafirishaji wa magari kwa asilimia 40% ili kurahisisha watu kuweza kuagiza magari yao toka UK kwa bei nafuu. Pia tutakuwa tunatoa free storage kwa magari na free loading. 
 Kama kuna mtu ana kitu au mzigo ndani ya ofisi zetu za sasa tunaomba aje achukue sababu hatutahama na mzigo wa mtu 
 Wote mnakaribishwa. 
 CHRIS LUKOSI 
 Managing Director SERENGETI FREIGHT


WE ARE OPEN ON SATURDAY 10:00-18:00HRS
WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

CHRIS LUKOSI +44 (0) 790 38 28 119 OR  +44 (0) 7404 27 96 33
SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. HONGERA SANA. NAWAPONGEZA SANA KWA KUJIKWAMUA NA KARAHA HII YA KUBEBA MABOX NA HAWA NDUGU ZETU WA KUTOKEA KULE NANILII KARIBU NA UKRAINE

    ReplyDelete
  2. WAZEE WA KAZI.

    ReplyDelete
  3. Hawa ndio wa kupewa....pacha na sio wale wagaagaa...kutwa kulialia....

    ReplyDelete
  4. mweusi wa kwanza TILBURY PORT ANAITWA FABIAN(ZIMBWABWE),BUT KEEP IT UP UR DOING GOOD JOOB WAZEE WA KAZI

    ReplyDelete
  5. Wabongo kwa wivu!! Ndo maana hatuendelei sasa akiwa mzimbabwe sisi tufanye nini??hovyoo!

    ReplyDelete
  6. Fabian ni half cast wa kizungu

    Baba yake Fabian ni mzungu muingereza pure aliekwenda Zimbabwe kuwekeza.

    Mimi ni mhehe mweusi kama mkaa natokea Kalenga, baba na mama wote wahehe wa Kalenga..

    Upo hapo ANONI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...