Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiingia  kwenye ukumbi wa mkutano  wa Town Hall ambao baadaye yeye na viongozi vijana wenzie watakutana na Rais Barak Obama wa Marekani  atakapozungumza nao  jijini Washington DC.
Hii ni sehemu ya program ya mafunzo kwa viongozi wadogo walioonyesha dira toka nchi zote za Afrika (most promising young African leaders) . Program hii imeanzishwa na Rais Obama mwenyewe.
Miongoni mwa watanzania wachache waliopata fursa ya kuhudhuria ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Steven Masele na Mhe. Joshua Nassari. Watakutana pia na Waziri wa mambo ya nje wa marekani John Kerry na Mke wa Rais Obama Bi Michelle Obama Pamoja na maseneta, Magavana, wafanyabiashara wakubwa an watu wengine mashuhuri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...