Mmoja  kati ya  waumini  wa dini ya Kiislam  wa madhehebu ya Answaar Sunna iliyofanyika katika  uwanja  wa Mwembetogwa akitoka kuswali  Swala ys Idd leo katika  uwanja  wa Mwembetogwa  mjini  Iringa
 Sheikh Dhulkifilo Omari  kulia akiwa na baadhi ya  waumini mara baada ya  ibada  ya Idd el Fitr   leo katika  uwanja  wa Mwembetogwa  mjini  Iringa
..............................................................................
Na matukiodaimablog
Sheikh wa  msikiti  wa  Hidaya katika manispaa ya  Iringa  Dhulkifilo Omary  wa  amempongeza  Rais  Jakaya Kikwete  kwa jitihada zake  kubwa  za  kufanikisha Tanzania  kuanza mchakato wa  kupata katiba mpya na  kuwaonya wajumbe wa bunge la katiba  kurejea bungeni kuunda katiba iliyo bora badala ya  kuendeleza mivutano isiyo na tija.

Akizungumza  leo  mara  baada ya   swala ya  Idd  el Fitr  kwa  waumini  wa madhehebu ya Answaar Sunna iliyofanyika katika  uwanja  wa Mwembetogwa  mjini  Iringa Sheikh  Omary  alisema  kuwa  kazi kubwa na nzuri  imefanywa na  Rais  Kikwete katika kuanzisha  mchakato wa katiba  ikiwa ni  pamoja na kuunda tume ya katiba na hadi  kufanikisha rasmu  hiyo ya katiba.
Hivyo  alisema  kuwa  wajibu  wa  wajumbe wa  bunge la katiba na kushiriki  kuandaa katiba ambayo italetwa kwa  wananchi kwa  lengo la  kuipigia kura  na  si  wakati wa  wajumbe hao  kuanza mivutano  isiyo kuwa na  tija  .

" Mimi  kwa  mawazo yangu  mimi kama sheikh  Omary  hawa  wajumbe  wa  bunge la katiba  walipaswa  kuketi  pamoja  bunge na  kutuletea katiba  nzuri na  sio  kutuletea  vurugu na malumbano  yasiyo kwisha  katika  bunge  hilo"
Alisema  kuwa vurugu  zinazoendelea  juu ya katiba   hiyo kwa  wajumbe  kuwa katika makundi makundi ni  wazi kuwa hakutakuwa na katiba mpya kwa  sana   iwapo makundi  hayo yataendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...