Kinyang’anyiro cha mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa na kituo cha televisheni cha East Africa(EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania,yanaendelea ambapo hapo kesho hatua ya robo fainali inafanyika katika uwanja wa Don Bosco Mbuyuni Namanga jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi 16 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es Salaam.

Makundi ya wachezaji wa miondoko mbalimbali ya muziki ambao yamefanikiwa kuingia ngazi ya robo fainali ni Wazawa Crew,Best Boys Crew,G.O.P,The W-T,Best Love,Tatanisha Dancers,Bustani,Quality Boys,Pambana Fasaha,Wakali sisi,Tamtam, Mazabe,TWC,B2K na Winners Crew.

Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha robo fainali hiyo watapata makundi 10 yatakayoingia moja kwa moja ngazi ya nusu fainali hapo baadaye.

“Huu ni mwaka wa tatu East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya kwa udhamini wa Vodacom Tanzania na kinywaji cha Grand Malta na mwaka hadi mwaka yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi ambao hujitokeza kushiriki”Alisema Shame.

Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5.

Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.

Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.

“Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu.

Aliwataka vijana waamke wasibaki nyuma na watumie fursa kama hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi “Suala la ajira sio kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia mapato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.
Vijana wanaounda Kundi la Mob Squad Kutoka Wilaya ya Temeke wakionyesha umahiri wao katika shindano la Dance miamia hivi karibuni,liloandaliwa na East Africa TV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Baadhi ya mashabiki waliofurika katika mashindano hayo hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...