Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif, (Wa pili toka Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni inayotarajiwa kuzinduliwa siku ya Alhamis Septemba 4, 2014 katika viwanja vya Leadrs Club. Pembeni yake ni Rais Wa Bongo Movie Steve Nyerere na wasanii wengine.

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
FILAMU ya ‘Mateso Ughaibuni’ ambayo imerekodiwa Uingereza na wasanii Issa Musa ‘Cloud 112’, Riyama Ally, Wastara Juma na Monalisa itazinduliwa Alhamisi hii katika viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif, ambaye kampuni yake ndiyo iliwapeleka wasanii hao Uingereza kwenda kurekodi filamu hiyo, alisema licha ya kampuni yake kujihusisha na mambo ya mavazi na vitu vingine ameona kuna kila sababu ya kuwasaidia Watanzania wanaofanya sanaa ya uigizaji.
Rais wa Bongo Movie Steve Nyerere akiongea machache mbele ya waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif na Flora Mvungi.

Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini.
Wafanyakazi wa PSPF nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nadhani itakuwa imetowa somo na fundisho tosha, khususan kwa wanaodhani ughaibuni ni raha tupu kwa kwenda mbele, kumbe nako kuna madhila yake na khasa mambo yanapokwendea mrama na kujikuta ungali mgeni na miji ya watu huku ukijiuliza ni wapi pa kukimbilia au nani wa kumwendea, roho na imani za watu hubadilika na kuwa tofauti na wale uliokuwa ukiwadhania mwanzo. Hongereni sana waandaaji, wahusika na washiriki wote katika movie hii ya 'MATESO YA UGHAIBUNI'. Am dying to watch it.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...