Hussein Ali Salum a.k.a CHINA azungumza kwa ufupi kuhusu Historia ya Maisha yake. pia aliongea kuhusu mchezo aliokuwa akiupenda wa mpira wa vinyoya yani Badminton Net na kutaja baadhi ya wachezaji waliokuwa bora katika timu ya Taifa ya Zanzibar Badminton kwa mchezo huo enzi zake, na pia aliongea kuhusu alivyosafiri na kuwa Baharia na kutembea nchi tofauti mwaka 1987. Na pia kutoa ujumbe kuhusu waTanzania kwa ujumla wanaoishi maisha ya Ughaibuni kuangalia wazee wao na kuekeza nyumbani kwa ujumla Jiunge nasi kwa kusikiliza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Shukran sana muandaaji wa mahojiano hayo, binafsi huyu Bw. China nlikuwa nikimuona tu pale bandarini DSM. Sometimes utamuona akirandisha peremende zake za biashara kwa abiria wanaosubiri usafiri wa kwenda Z'bar, huku akitudhihaki kwa 'uchepe' huu na ule huku tukivunjika mbavu kwa kucheka khususan akianza ile lafdhi yake ya 'kichinachina'. Lakini leo si haba nimeweza kuisikiliza kwa kituo 'interview' yake na kaweza kujieleza kwa ufasaha kabisa. Mwisho nazidi kukuombea kila la kheri Bw. China katika harakati zako za kila siku katika kupambana na maisha. Nimefarijika sana ulipoelezea historia yako katika suala zima la 'kutarazaki' khususan humo mote ulimojaaliwa kufika, lakini end of the day umeliweka bayana na kukiri kuwa...kupata kuna Mungu. Basi In Sha Allah, nazidi kukuombea kila jema na Mola akujaaliye maisha mazuri ya salama, amani na furaha tele. Pongezi za dhati kwa mtangazaji aliyeandaa mahojiano hayo Bw. Abuu na Swahili Vila kwa jumla.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...