Ni matumaini yangu kuwa nyote muwazima na sie hatujambo huku Bondeni Sauzi.
Maudhui ya barua hii ni kukufahamisheni kuwa kuna Mtanzania kwa jina Shukuru Goyagoya kafariki tarehe 16th mwezi huu katika Hospitali ya Baragwana Jo'burg.
Alikua Kalazwa ICU takriban mwezi mmoja.

Hapa Sauzi alikuwa akiitwa kwa jina la umaarufu Jastice Mliambe Manesi kazaliwa mwaka 1970.

Maelezo niliyoweza kupata, Mama yake mzazi anaitwa  Bi Ziada Musa Kitima anaishi Mabibo CCM . Naomba msaada wenu wa kutangaza katika chombo chako habari hii ili jamaa zake marehemu taarifa hii iweze kuwafikia popote pale walipo. Na taarifa hii nimeweza kuifikisha katika Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria

Mpaka sasa maiti bado ipo Hospitalini tunasubiri uamuzi wa pamoja ikiwa marehemu azikwe hapa Jo'burg au maiti yake isafirishwe hadi nyumbani kwao. Nashukuru kwa msaada
Wenu. Kila la kheri

Omar Mutasa
BBC
Joburg

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. R.I.P.... Hongera bwana Omari kwa juhudi zako.....mungu atawalipa kwa hilo....

    ReplyDelete
  2. Inna Lillah Wainna Ilayhi Rajiun. Mola amlaze pema na amnusuru na adhabuze - AMEEN.

    Hongera sana Bw. Omar Mutasa, Mwenyeez Mungu akujaze kila la kheri. Shukran za dhati kwa juhudi zako za kutukhabarisha, In Sha Allah, tunaimani ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wataweza kupatikana na kujitokeza once watakapozipata khabari hizi na kupitisha maamuzi yao ya pamoja, juu ya nini kifanyike kuhusiana na mazishi. Poleni nyote mliofikwa na msiba huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...