Na Sultani Kipingo
Habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Bi Julia Pierson (pichani) , Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Rais wa Marekani maarufu kama Secret Service, amejiuzuru nafasi hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wan chi hiyo  Bw. Jeh Johnson ametangaza leo. Katika taarifa yake Bw. Johnson kasema atamteua Bw. Joseph Clancy kukaimu wadhifa huo nyeti.
Afisa habari wa Ikulu ya Marekani Bw.  Josh Earnest amesema katika mkutano na wanahabari leo kuwa Rais Barack Obama alimwita Bi Pierson na kumshukuru kwa utumishi wake katika Idara hiyo na nchi ya Marekani, na kwamba Rais huyo aliweka bayana kwamba iko haja ya kuwa na uongozi mpya katika Idara hiyo.
Akiongea baada ya uamuzi huo wa kuachia ngazi, Bi. Pierson alisema ulikuwa ni uamuzi mchungu. “Nadhani (uamuzi huo) kwa maslahi ya Secret Service na umma wa Wamarekani.  Congress (Bunge) limepoteza imani name kuongoza Idara hii. Vyombo vya habari navyo vimeweka bayana kuwa hili ndilo wanalotarajia. Ni uchungu kuacha kazi katika Idara hii ambayo inaandamwa na kashfa mbalimbali za uwajibikaji mbovu wa usalama”.
Bi Pierson alikuwa amekalia kuti kavu na kuwekwa katika hali ngumu kufuatia matukio kadhaa ya kuhatarisha usalama  (wa Rais), ikiwa ni pamoja na mtu mmoja kuruka uzio wa White House na kuingia ndani akiwa na kisu mkononi mnamo Septemba 19 mwaka huu. Inaripotiwa kuwa aliingia humo ndani baada ya kumzidi nguvu afisa usalama aliyekuwa lindo, kabla ya kuzidiwa nguvu na afisa mwingine aliyekuwa amemaliza zamu.
Baada ya tukio hilo, matukio mengine ya kuhatarisha usalama wa Rais yakaibuka. Moja likiwa ni kuruhusiwa kwa mtu mmoja aliyewahi kufungwa jela kuingia katika lifti moja na Rais Obama alipokuwa akizuru Taasisi ya kuzuia magonjwa mwezi uliopita. Pia kuna tukio la mtu kupiga risasi Ikulu hiyo ya Marekani ambayo pia ni makazi rasmi ya Rais wa Marekani.
Jumanne iliyopita Bi Pierson aliwekwa kitimoto na kamati ya Bunge kuhusu matukio hayo. Alisema tukio la karibuni lilikuwa halikubaliki na akakiri udhaifu wa idara katika majukumu yake. “Nakubali kubeba lawama zote”, alisema. “Haitotokea tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ahhhgh..kawaida hata bongo wanajiuzuru sana tu viongozi wetu ....tena hata bila ya kuwepo shinikizo........

    ReplyDelete
  2. usala wa taifa wa marekani michuzi.

    ReplyDelete
  3. Huu ndiyo unaitwa uwajibikaji utendaji ukiwa na kasoro katika ofisi yako unatakiwa kujiuzulu hata kama hukushiriki. Hii inasaidiaa wafanyakazi wawe makini kuhamasisha kazi katika ofisi zao.

    ReplyDelete
  4. Anonymous 1 unayoyasema ni kweli? How many times watu wanang'ang'ania vitengo japo vinawashinda?Bongo kuachia ngazi,kukubali kushindwa ni SHIDAAA!

    ReplyDelete
  5. Bongo hakuna uwajibikaji,swala la kujiuziru ni ndoto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...