Usiku wa Oktoba 21 ni siku yangu muhimu sana kwani, ndiyo niliyozaliwa. Hii ilikuwa ni majira ya saa 3 usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni mwaka 1985.
Leo nina furaha isiyo kifani kwa kuweza kusherehekea  siku yangu hii ya kuzaliwa… hakika Mungu ni mkuu nawashukuru nyote kwa kushirikiana nami bega kwa bega katika kipindi chote cha maisha yangu nawatakia kila lakheri pia.
Najivunia kua mtanzania ila ndani  ya miaka hii yote  nakumbuka mengi na nimepitia mengi ikiwemo milima na mabonde machozi na jasho la damu.
Kwa kifupi, mpaka kufikia leo tokea 1985,  lakini hapo hapo natimiza miaka 14 ya mateso katika uhai wa kuishi  pekee yangu (kujitegemea) ni hakika naeleza nimepitia mateso makubwa huku kubwa kuliko ni la kuishi katika maisha ya mtoto wa mitaani (Street children) lakini Mungu alikua nami na wasamalia wema wakanitoa huko na sasa nipo hapa nilipo.
Hivyo kwa mateso niliyopitia kwa zaidi ya miaka hiyo  hiyo 14,  na leo  hii kuona mwaka huu.. ni faraja sana kwangu na namshukuru Mungu kwani bado yupo na mimi siku zote na hakika matunda yake nayaona mbali ya kuwa na vikwazo vingi mbele yangu.
Hivyo basi leo nawashukuru nyote kwa kua nami bega kwa beka kwa kipindi hiki na kijacho shukrani ziwafikie wote wakiwemo kwa uchache Bosi wangu, Ansbert  Ngurumo, (Freemedia Ltd), Mohamed Dewji (MB-Singida mjini), famlia ya Mnyanga, Simtoe, Mtweve, Munaar, Wafanyakazi wote wa Freemedia Ltd * Tanzania Daima na Sayari, wafanyakazi wenzangu na wanachama wa kikosi cha maafa na uokoaji Tanzania Red cross, Shyrose Bhanji, Agustino Chale (baba mkubwa) Living Faith Church, familia ya Monga, wanafunzi wote Gilman Ruthinda primary LY 2002,  wanafunzi Sekondar- Mbalizi High  na Meridian High  ... bila kuwasahau wanafunzi wa Royal Collage of Tanzania, Red Cross Tanzania First Aids Collage na wengine wengi nyote nawashukuru sana I say  I love all..and Blogger nyote nawashukuru
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...