Makampuni yanatengeneza / toa bidhaa/huduma, wateja wanatengeneza brandi

Makampuni yanatengeneza bidhaa au kutoa huduma zenye majina ambazo hununuliwa na wateja, ila brandi huja kutokana na muono, matarajio na hata uzoefu wa wateja.
Mfano, bidhaa za Toyota ni magari, brandi kuu wanayotumia ni Toyota, na kwenye kila bidhaa zao huwa na brandi nyingine zinazotofautiana kulingana na mifumo yake, mfano Toyota Hiece, Toyota Prado nk, hivyo Prado ni brandi ndogo ya brandi kubwa Toyota. 
Toyota wanatengeneza magari ila Prado ni gari la toyota leye sifa fulanifulani kulingana na uzoefu wa wateja. Uzoefu huu unaotengenezwa na watumiaji ni lazima utoke kwa muuzaji bidhaa (Nini cha kipekee kwenye bidhaa / huduma yako? , nini unataka wateja wakipate kwenye bidhaa / huduma?). Kumbuka, wateja hawanunui bidhaa, bali kitokanacho na bidhaa na hiki ndicho kitatengeneza brandi yako.Hivyo ni lazima ukidhi matakwa / mategemeo ya wateja toka kwako. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...