Mkurugenzi Mtendaji Wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC),Juliet Kairuki (kushoto) akizungumza machache katika mkutano baina ya TIC na uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ulioambatana na kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika kupeana taarifa na takwimu ambao utakuza maslahi ya kiutendaji katika taasisi hizo.Wa pili kushoto ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC),Juliet Kairuki na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade wakisaini mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kupeana taarifa na takwimu,ikiwa ni mpango utakaozipatia maslahi taasisi hizo.Mkataba huo ulisainiwa mwishoni mwa wiki kwenye Ofisi za TIC,jijini Dar es Salaam.Wengine pichani toka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Nakuala Senzia,Mwanasheria wa TIC,Alex Mnyami,Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa TIC,Pascal Maganga,Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti wa TIC,Anna Lyimo pamoja na Mkurugenzi wa Elimu kwa Walipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC),Juliet Kairuki na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Rished Bade wakibadilishana mikataba hiyo mara baada ya kuisaini, kwenye Ofisi za TIC,jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa wa Kituo cha TRA ndani ya TIC,Adam Lingwetu (kulia) akifafanya jambo juu ya machine maalum ya kutoa Namba za TIN wakati wa mkutano baina ya TIC na uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za TIC,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...