Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Morogoro, Bi Anna Wesiwasi (wapili
kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Kituo cha Amani cha watoto wenye
ulemavu, Padri Beatus Sewando (watatu kulia) mara tu baada ya kuzindua
jengo la kituo hicho kilichokarabatiwa na benki hiyo jana mkoani
Morogoro. Akishuhudia ni Afisa Mauzo wa Benki hiyo Vick Haji (Kulia).
Na Mwandishi wetu, Morogoro
BENKI
ya Exim Tanzania imefanya ukarabati wa majengo ya kituo cha watoto
wenye ulemavu cha Amani kilichopo eneo la Chamwino mkoani Morogoro ikiwa
ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuboresha maisha ya jamii.
Kupitia
sera yake ya kurudisha sehemu ya faida yake kwa jamii, benki hiyo pia
imejipanga kutoa misaada zaidi ikilenga mipango yenye kuleta maendeleo
kwa jamii hapa nchini hususani katika maeneo ambayo benki hiyo tayari
imefungua matawi yake.
Akizungumza wakati wa
hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya ukarabati wa majengo ya kituo hicho
iliyofanyika mkoani humo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa tawi la
benki hiyo mkoani Morogoro, Bi Anna Wesiwasi alisema msaada huo pia
unalenga uboreshaji wa maisha ya watoto wanaoishi kwenye kituo hicho kwa
kuwa wataishi kwenye makazi salama, safi na bora kwa afya zao.
“Benki
ya Exim siku zote tunaamini kuwa watoto wenye ulemavu wanahitaji kupewa
matumaini zaidi na kwa kushiriki kwetu kwenye mipango ya maendeleo kama
huu ndio tunatekeleza hiyo imani yetu kwa vitendo na zaidi tunazidi
kuwa karibu na jamii inayotuzunguka jambo ambalo ni muhimu katika
ulimwengu wa kibiashara kwa sasa kuona kwamba benki inarudisha sehemu ya
faida yake kwa watu inao wahudumia,'' alisema Bi Wesiwasi
Kwa
mujibu wa Bi Wesiwasi, benki hiyo inaamini kuwa watoto ndio wateja wao
wa kesho kama sio wa sasa na hivyo basi benki hiyo itajitoa kwa hali na
mali kuhakikisha kwamba wanapata maisha bora kwa sasa .
Akizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi wa kituo hicho, Padri
Beatus Sewando alisema uamuzi wa benki hiyo kusaidia kituo cha watoto
wenye ulemavu ni kitendo kinachotakiwa kuigwa na taasisisi, mashirika na
watu mbalimbali hapa nchini.
“Tunashukuru sana
kuona wenzetu wa benki ya Exim wameonyesha mfano kwa kuitikia kilio
chetu.Msaada huu utawahakikishia watoto wetu hapa kituoni kuwa na
makazi bora na salama kwaa afya zao…naomba wengione waige mfano huu,’’
alitoa wito
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...