Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini amezindua usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua, Rex Energy, inayotarajia kuzifikia kaya milioni moja na nusu kufikia mwaka 2020 kupitia teknolijia mpya ya umeme wa jua wa gharama nafuu. 
 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa teknolojia hiyo mpya inayojulikana kama 3G+ Solar Home System (SHS) iliyobuniwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ikiwa ni mara ya kwanza kutumika Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Rex Energy Francis Kibhisa lengo la mradi huo ni kuwafikia watanzania wengi zaidi Teknolojia hiyo ya kisasa imebuniwa na mshirika wa Rex Energy, Kampuni ya Nishati ya Solaric Pvt Ltd yenye makao makuu nchini Bangladesh. Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa teknolojia hiyo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
Bw. Kibhisa alisema; “Rex Energy imefanikiwa kuwa mbele katika utoaji wa bidhaa bora zilizo suluhu ya soko la nishati ya jua na kwa kuzindua 3G+SHS leo, nawahakikishia wateja wetu bidhaa bora ya SHS kwa mahitaji yao ya jumla.” Teknolojia hii imejaribiwa nchini Bangladesh, India na Malaysia na nina uhakika ni suluhisho kwa maeneo yasiyofikiwa na gridi vijijini nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwa mpango wa muda wa kati,” alisema. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Bangladesh alisema: “Kwa uvumbuzi wa 3G+SHS, gharama za SHS zimepunguzwa na kadhalika mahitaji ya kuihudumia kwa kiasi kikubwa na kuifanya bidhaa hiyo kuwa yenye faida kibiashara.
“Rex Energy iliteuliwa kuwa mshirika wetu kwa sababu ya rekodi yao nzuri katika sekta ya nishati ya umeme wa jua na uwezo wao wa kulifikia soko,” alisema. 
 Uzinduzi wa 3G+SHS pia unatoa suluhu ya masuala ya kuimudu bei, ambayo yamekwamisha watu wengi walio nje ya umeme wa gridi kunufaika na nishati. “Tuna mfumo wa malipo, ambao unaruhusu wateja kulipa amana na kiasi kilichosalia kulipwa kipindi cha miezi 12 ili kumsaidia mteja kutobeba mzigo wa kulipa mara moja,” alisema. 
 “Huu ni mfumo wa lipa kadiri ya unavyotumia (PAYG), ambao mteja anamiliki mfumo wa umeme wa jua baada ya kumaliza kulipa sehemu ya fedha iliyobakia. Bidhaa pia imetengenezwa kwa namna ya kuendana na mahitaji ya makundi tofauti ya jamii za vijijini na hata za mjini kwa vile inakuja kwa ukubwa tofauti linapokuja suala la uwezo wa nishati ukihusisha kuanzia matumizi ya mwanga na kuchaji simu hadi kuwezesha vifaa vya umene kama vile runinga; feni, kompyuta mpakato na kadhalika,” Kibhisa anasema 
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS). Katikati ni Paul Kiwele Naibu  Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini,Mwisho ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam.
Mgeni rasmi katika uzinduzi  wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele katikati akizindua teknolojia hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam
Injinia Arnold Swai wa Kampuni ya Rex Energy akionyesha namna  Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) inavyofanya kazi. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele.
Waandishi wa habari waliojishindia seti ya mfumo mpya wa umeme jua ujulikanao kama  3G+Solar Homes System (SHS) kwenye droo iliyochezeshwa wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam jana. Wa kwanza kulia (waliovaa suti) ni   Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam alikifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na mgeni rasmi katika uzinduzi huo Paul Kiwele ambaye ni Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...