Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na kusaidia  watu wenye  mahitaji maalum (SVF) limesema watu wenye ulemavu wako milioni 4.5 lakini wanakabiliwa na changamoto kutokana na mazingira wanayoishi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa shirika hilo,Leontine Rwechungura amesema kutokana na kutambua mahitaji ya kundi la watu wenye ulemavu,wataanza kujenga miundombinu rafiki kwa wanafunzi katika shuke ya Sekondari, Jangwani,Pugu  na shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko.

Alisema watu wenye ulemavu wakijengewa mazingira rafiki wanaweza kuondokana na changamoto na taifa kupata wataalam wanaotokana na kundi hilo.

“Serikali imeweza kufanya na inaendelea kufanya lakini kama taasisi tunawajibu wa kufanya kutokana na wote ni jamii moja lakini wamepata ulemavu”alisema Rwechungura. 

Naye Mwakilishi wa Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam (REO),Benardetha Thomas alisema kuwa vitu ambavyo taasisi hiyo imeahidi itekeleze kutokana na watu wengine wanaahidi na hawatekelezi.
 Katibu Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na kusaidia  watu wenye  mahitaji maalum (SVF),Leontine Rwechungura akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wao uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo,jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika hilo,Frad Kaula na kulia ni Meneja Uhusiano wa Shirika hilo,Urith Mjema.
Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na kusaidia  watu wenye  mahitaji maalum (SVF),Frad Kaula akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wao uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo,jijini Dar es salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia Mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...