Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli
kushoto akizungumza jambo na Mbunge wa Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mhe Freeman Mbowe wakati Waziri wa Ujenzi
alipokagua barabara ya Kwa sadala-Masama-Machame JCT km 16.
Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Pombe Magufuli kushoto akimtaka mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe
kuchangia shule mojawapo iliyopo Masama kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa pamoja
na mabweni.
Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Mhe Freeman Mbowe katikati
akiwa na Diwani wa kata ya Masama Ali Mwanga wakimpigia makofi Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuchangia shilingi milioni tano kwa
ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa na mabweni katika shule ya Sekondari
Kokashu iliyopo katika Kata hiyo ya Masama. Mbunge wa Hai, Mhe Freeman Mbowe naye alichangia
kiasi cha Shilingi milioni tano.
Mbunge wa Hai mkoani
Kilimanjaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi wakicheza kwa furaha pamoja na
wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliohusu ujenzi wa barabara ya Kwa
sadala-Masama-Machame JCT km 16.
Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Magufuli akiangalia nyufa ndani ya jengo la Wilaya ya Siha ambalo
lilisimamiwa ujenzi wake na Wakala wa Majengo Tanzania TBA. Waziri Magufuli
ametangaza kujengwa upya kwa jengo hilo mara baada ya kubaini kasoro mbalimbali
na ametoa muda wa wiki mbili kwa Wakala kuhakikisha wanaanza kazi hiyo.
Chadema wako juu sana aisee, ila sifa nyingi zitawalevya na kua kama cuf
ReplyDeleteTanzania ijayo ikiwa Ina kiongozi mkuu anayefanya kazi zake kwa weledi bila itikadi za vyama na woga Kama MHE. MAKUFULI nchi itakuwa mbali Sana. Mungu tusaidie !!
ReplyDelete