Othman Khamis Ame, OMPR -  ZNZ
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alionya kwamba wananchi wanalazimika kujenga utamaduni wa kuthamini kazi za wabunifu na wasanii kwa kuona fahari kuzilipia bila ya shuruti pale wanapozitumia jambo ambalo ni uungwana na kinyume chake inahesabika kuwa ni wizi. 
Alisema Serikali kupitia Ofisi ya Hakimiliki, Bodi ya Hakimiliki na Jumuiya ya Hakimiliki Zanzibar { COSOZA } itaendelea kusimamia kazi za wabunifu na wasanii ili kuona kuwa maslahi, nguvu na jasho lao halipotei bure kutokana na ulaghai unaoendelea kufanywa na watu wanaozipora kazi zao. 
Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati wa hafla ya ugawaji wa Mirabaha kwa Wabunifu na wasanii Zanzibar zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar. 
Alisema Serikali itaendelea kuchukuwa hatua za kisheria za kuwadhibiti wezi hao wasiojali jasho la wenzao, lakini kazi hiyo inaweza kufanikiwa kwa ufanisi zaidi endapo wabunifu na wasanii wenyewe watatoa ushirikiano kwa taasisi zinazosimamia maslahi yao katika kudhibiti wizi wa kazi zao. 
Alifahamisha kwamba Serikali haipendi kuwabughudhi wananchi wake katika biashara hata kidogo lakini hulazimika kuchukuwa hatua za kisheria mara moja pale ambapo uvunjaji wa sheria unapobainika ili haki ipatikane kutokana na sheria inavyochukuwa mkondo wake. 
Akitoa Taarifa Msimamizi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Hakimiliki Zanzibar Bibi Mtumwa Khatibu Kheir alisema huo ni mgao wa pili wa Mirabaha kwa wabunifu na wasanii wapatao elfu 1124 wa zanzibar. 
Bibi Mtumwa alisema Ofisi ya Hakimiliki imefanya kazi kubwa na nzuri kwa kushirikiana na kamisheni ya Utalii pamoja na Mamlaka ya Uwekezaji vitega uchumi Zanzibar { ZIPA } katika kuziunganisha kwa wateja kazi za wabunifu na wasanii. Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi Balozi Seif, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis Bakar alisema vipaji walivyokuwa navyo wabunifu na wasanii wa Zanzibar ni vyema vikaenziwa na kuheshimiwa kwa faida ya Taifa kwa jumla.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi   wa Kamati ya ugawaji Mirabaha pamoja na washindi mbali mbali wa tuzo za wabunifu na wasanii bora kwa mwaka huu mara baada ya kukamilika jkwa sherehe hizo hapo Ukumbi wa Salama  Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.

Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis,Msanii Khamis Juma, Msanii Mwapombe Hiari na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo.

Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali M,barouk, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi, Mjumbe wa Kamati ya Ugawaji Mirabaha Mh. WEanu Hafidh Ameir pamoja na Mchangiaji bora wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh. Mahadh Juma Maalim. Picha na – OMPR – ZNZ.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...