Ndugu,

Ninafuraha isiyokadirika kwa hatimaye kufanikisha kazi niliyoianza takriban miaka minne iliyopita kuandika kitabu kinachoainisha mawazo yangu juu ya Tanzania tuitakayo, Tanzania ya mabadiliko, Tanzania ya mapinduzi kuelekea kupata maisha bora kwa kila mtu. Ndani yake nimejaribu kuelezea, kwa kadri nilivyojaaliwa, jukumu la kizazi chetu ni nini haswa? Misingi ya ukombozi wa kiuchumi na kijamii ni ipi haswa? Nini chanzo cha umaskini na utajiri wa nchi? Nini kifanyike ili tuvune na kufaidika na utajiri tulionao? Nini vipaumbele na mbinu za ukombozi tunaoutaka sana sasa? Ni nini yanapaswa kuwa mabadiliko tunayoyatarajia? 

Katika kitabu hiki naweka mapendekezo ya mfumo mpya wa kuendesha uchumi kwenye nchi zinazoendelea za Afrika kutokana na misingi ya utamaduni asilia wa kiafrika, nazungumzia nguzo nane za mfumo huu, ambao nimeuita 'African Socialism with Capitalist Characteristics'. Kanuni hizi zilizosheheni muundo wa fikra zangu, uliwahi kuitwa 'Kigwanomics' na rafiki yangu Michael L. Wilson (Ph.D.) wakati tukijadili mambo mbali mbali ya kiuchumi na mustakabali wa Africa tunayoitaka akiufananisha na mawazo ya watu wengine mashuhuri duniani waliowahi kusimamia mabadiliko kwenye nchi zao na kufanikiwa, kama Ronald Reagan (Reaganomics) ama Thaksin Shinawatra (Thaksinomics). Nami nilipenda kuazima style hii na kukiita kitabu changu, Kigwanomics.  

Katika kitabu hiki utasoma uchambuzi wa mawazo ya waandishi mashuhuri duniani kama akina Mchumi Prof. Paul Collier (The Bottom Billion n.k.), Dr. Chika Onyeani (The Capitalist Nigger), Why Nations Fail (Drs. Robertson and Acemoglu), What went wrong with Africa (Roel van der Veen), Dead Aid (Dr. Dambisa Moyo), Towards the African Renaissance (Prof. Cheikh Anta Diop) na wasomi wengine wa Africa.  

Imani yangu ni kwamba nimetoa changamoto ya namna mpya ya kufikiria juu ya mapinduzi ya upili (Secondary revolution) kuelekea Tanzania iliyozaliwa upya (Tanzanian Renewal). Lengo kuu la mawazo yangu kwenye kitabu hiki ni hili. Kama ukisoma na ukaona upya wa mawazo yangu, na haja ya kuiunda upya Tanzania Tuitakayo basi nitakuwa nimefanikiwa. 

Kitabu kitazinduliwa rasmi taratibu zitakapokamilika na tutakujulisha. Nimeandika kitabu changu kwa lugha ya kiingereza, na tayari kuna timu, inayoongozwa na Ndg. Prince Bagenda, inafanyia kazi tafsiri ya kiswahili, na kuna wataalamu wanaofanya kazi ya kuandaa 'popular version' ya kitabu hiki kwa lugha ya kiswahili ili kufikisha mawazo haya kwa haraka na kwa watu wengi zaidi. Ikikamilika kazi hii ndipo tutatangaza siku, mahala na saa ya kukizindua rasmi. Kwa sasa kinauzwa kwa bei ya 'promotion' ya TZS 5,000 kwa kila nakala, kwenye maduka ya TPH Bookshop na maduka yote ya Uchumi Supermarkets, Mlimani City (MAK Bookshop), pia kipo kwenye mikono ya wamachinga kwenye njia panda zote kubwa za jijini Dar es salaam, kimefika Iringa (Lutengano Investment), Vyuo Vikuu vyote iringa, Dodoma na Mwanza (Pia Kwa Ibrahim Campbell jirani na CRDB Mwanza Branch). 

Nakutakia usomaji mwema. Natanguliza Shukrani zangu za dhati na fanaka. 

Wakatabahu,
Hamisi Kigwangalla.
Mwandishi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera Dr! Kama ikwezekana, naomba utupatie link ya pdf version ya kitabu chako kama Ndugu Makamba alivyofanya.

    ReplyDelete
  2. Nakupongeza kutumia muda mwingi kuandika kitabu kwa lengo lakufanya mabadiliko chanya ktk nchi yetu; lakini kabla yakufika huko kwenye vitabu! Kutokea ulipo kua mtu mzima ukamaliza elimu yko ukapata nafasi nyingi na kubwa nchini umefanya kipi jitihada gani kudhihirisha hicho ulichokiandika leo? yaani kama ni African Socialism na viji element vya ubepari hatukatai!!! lakini ww ulifanya nn ulijitahidi kiasi gan kulisema kulifikisha serikalini au kulihubiri bungeni au kwenye vyombo vya habari au majukwaa yakisiasa uliyowahi kusimama!! Nyerere alipo andika Freedom and Unity alimaanisha alichokua anaandika kwa vitendo, alipokua akiandika Ujamaa na elimu yakujitegemea ilikua tu kuweka kumbukumbu ya yale aliyoyasimamia ktk maisha yke yote!!!! Msomi mwafrika, mwafrika mwanasiasa miaka hii ni watu wakuogopwa kama ukoma, wanachosema na kuandika ni kinyume cha maisha yao yakweli katika mioyo yao. Tutakisoma!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Kigwangala. Ni muhimu sana kuweka mawazo kwenye maandishi. Hatuishi milele.

    ReplyDelete
  4. Nunajifunza vingi sana kutoka kwako mheshimiwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...