Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akilakiwa na Dkt. Martha Kisanga, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Shirika la Engender Health mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Shule ya Sekondari Kibasila kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya siku 5 yaliyohusu mradi wa kuzuia mimba za utotoni katika Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke tarehe 17.4.2015. Waliosimama katikati ni Ndugu Donald Siliva, Afisa-Elimu Sekondari, Wilaya ya Temeke na Dkt. Sarah Maongezi, Mkurugenzi wa Afya kutoka Taasisi ya WAMA.
Meneja wa Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wana wake na Maendeleo, Ndugu Philomena Marijani akitoa maelezo ya awali kuhusiana semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke iliyofanyika huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akitoa hotuba ya kufunga rasmi mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari za Wilaya ya Temeke yaliyofanyika Kibasila Sekondari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...