Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
BOHARI ya dawa (MSD) imeboresha huduma kwa wateja
wake kwa kutoa taarifa zinazomhusu mteja kwa kuziweka
wazi katika tovuti yao.
Amesema hayo Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na
Shughuli za Bohari ya Dawa (MSD), Edward Terry,
akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa Habari
MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
Terry amesema kuwa taarifa hizo ni za mali
inayopatikanagharani, taarifa za kiasi cha fedha za wateja
kilichopo katika kila akaunti,fomu za marejesho pamoja na bei
za bidhaa na bei zake.
Pia Terry amesema kuwa wateja wenye mahitaji ya dawa au
vifaa wanatakiwa kuandika barua kuelezea mahitaji yao
pamoja na maelekezo mhimu ya kifaa husika na kutatuliwa na
kitengo cha manunuzi ya bohari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda
Bohari ya dawa (MSD), Edward Terry,akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa
habari MAELEZO jijjini Dar es Salaam leo kuhusu utendaji na
mipango ya Bohari ya Dawa (MSD) na Ofisa Uhusiano Mkuu wa
Bohari ya Dawa (MSD),Etty Kusiluka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...