MAKUNDI YA RCL
Jumla ya vituo vitatu vitatumika katika hatua ya makundi kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itakayoanza Mei 2 mwaka huu , vituo hivyo ni Lindi, Manyara na Sumbawanga huku kila kituo kikiwa na timu tisa;

Lindi ni Babati Shooting Stars (Manyara), Changanyikeni FC (Dar es Salaam), Coast United FC (Mtwara), FFU Football Club (Dar es Salaam), Kilimanjaro FC (Kilimanjaro), Matai FC (Rukwa), Sabasaba United FC (Morogoro), Small Boys (Singida) na Super Star (Pwani).

Manyara ni Alliance Schools (Mwanza), Bariadi United (Simiyu), Baruti FC (Mara), Lukirini FC (Geita), Madini SC (Arusha), Mtwivila City FC (Iringa), RAS Kagera FC (Kagera), Small Prisons (Tanga) na Watumishi FC (Shinyanga).

Sumbawanga ni Abajalo FC (Tabora), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Gunners FC (Dodoma),  Lucent FC (Ruvuma),  Market Place FC (Lindi), Mwanga United (Kigoma), Nyundo FC (Katavi), Tomato FC (Njombe) na Zakhem FC (Dar es Salaam).

Timu mwenyeji zimeondolewa katika vituo vyao na kupelekwa vituo vingine ili kuondoa masuala ya uzalendo, na kuhakikisha fair play inakuwepo.

Kila kundi lina timu tisa, na timu itakayoongoza kituo kwa mechi za ligi ya mkondo mmoja ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...