Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mkuu utafanyika kama ulivyopangwa na haiwezi kufanya uchaguzi huo usogezwe mbele kutokana na suala hilo kuwa la kikatiba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa wanasiasa wamekuwa na kauli ambazo zinawafanya wananchi wapate hofu wakati suala hilo kuhairisha uchaguzi halipo katika tume.

Amesema kuwa wanasiasa wametakiwa kuangalia maneno ambayo wanayatoa kwani hayana msingi kwani wanatakiwa watoe sera zao za vyama kwa wananchi na sio kuisemea tume mambo ambayo hayana ukweli wowote.

Amesema zoezi la kuandikisha kwa Mkoa wa Njombe ambalo linaisha kesho na kuhamia katika mikoa ya Iringa,Lindi,Ruvuma pamoja na Mtwara ambalo litaanza Aprili 24 mwaka huu.

Lubuva amesema wanatarajia kupokea vifaa vya kuandikisha kwa kuchukua alama za vidole (BVR)1600 ambazo zitafanya kazi katika mikoa hiyo na kuhamia Mikoa ya Dodoma,Mbeya,Katavi pamoja na Rukwa kuongezeka BVR tena 1600 na BVR 1,152 zitafanya kazi katika mikoa Singida,Tabora,Kigoma pamoja na Kagera na uandikishaji utaanza Mei 2 mwaka huu.

Aidha amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura litamalizika Julai mwaka huu hivyo wananchi wajiandae katika kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Jaji Lubuva amesema Rais Jakaya Kikwete anataka amalize ili apumzike hivyo hakuna mpango wowete wa kuongeza muda wa uongozi kwake.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Manunuzi na Logistic,Gregory Kaijage na kushoto ni Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama),Sisti Chriati.
Baadhi ya wandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...