Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao ulitaka kuwasilishwa bungeni kwa dharula. Kulia ni Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Comminication, Samuel Nyalla (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Saed Kubenea kutoka Mwanahalisi Publishers na Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akisalimiana kwa kumbatiana na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari.

WAMILIKI wa Vyombo vya habari nchini (MOAT) wameitaka serikali kutosaini muswada wa vyombo vya habari kutokana na kutokuwa wa haki na kwamba unavibana vyombo vya habari.

Pia wamiliki hao wamesema kama serikali inataka kuupitisha isubiri Rais ajaye ndiyo aupitishe wakati huohuo wameunda kamati maalumu itakayoenda Mjini Dodoma kuuzuia usipitishwe wala kujadiliwa bungeni.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi  alisema anashangazwa sana na wanasisa kusahau walipotoka kutokana na kusapoti muswada huo kupitishwa.

Alisema serikali imeamua kufanya hivyo kutokana na kusahau waliowasababishia kupata madaraka kutokana na shida yao kuisha hivyo vyomba vya habari vimejifunza.

"Tumejifunza kuwa sisi ni8 watu wa kutumika  wanapotaka kututumia hivyo wanataka kutumaliza na muswada huu hivyo sioni kama wana nia njema na sisi, "Alisema Mengi.

Aliongeza nia ya kupitishwa kwa muswada huo so njema na kwamba haki ya kupata habari sio tuu haki ya msingio bali ni ya kikatiba hivyo serikali isije ikajihusiasha na kuvunja katiba ya nchi bali inatakiwa kuonesha mfano bora.

HABARI ZAIDI SOMA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...