Na Dotto Mwaibale

NYOTA ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa yazidi kung'aa baada utafiti uliofanywa na Samunge Social Research Center na kugundua wananchi wengi kumpenda na kumuhitaji agombea urais wa mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mtafiti Mkuu wa Tafiti  hiyo George Nyaronga alisema baada ya Waziri huyo kudai kuwa atagombania wananchi wengi wameonyesha kumuhitaji kwa kiasi kikubwa.

Alisema katika utafiti huo walioufanya waligundua kuwa Waziri huyo mstaafu anaongoza kwa asilimia nyingi kuliko wenzake anaowafata.

Akitaja asilimia hizo alisema Edward Lowassa anaongoza kwa asilimia 20.7 akifuatiwa na Wilbroad Slaa asilimia 11.7, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (Chadema)Freeman Mbowe asilimia 3.4, Mwenyekiti wa Chama cha Wanachi CUF Ibrahim Lipumba asilimia 4.2.

Wengine ni pamoja na Waziri wa Ujenzi John Magufuli 7.6, Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba asilimia 4,Waziri Mkuu Mizengo Pinda asilimia 2.4,Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje Bernard Membe7.0 na Mwenyekiti wa chama cha Nccr Mageuzi James Mbatia 1.2.

Alisema kwa kutokana na nchi kuelekea katika uchaguzi wananchi wamekuwa na muamko wa hali ya juu katika kuhakikisha kila mmoja atapigapiga kura kwa mwaka huu.

"Tumefanya tafiti hizi na kuona kwamba watanzania wengi wameamua kuingia kwenye masuala ya siasa na kuleta mabadiliko katika nchi yao na si kupigiwa kura,"alisema.

Alisema kutokana na utafiti wao wamegundua kuwa wananchi wanahitaji rais ambaye ni muadilifu, msema ukweli, mwenye afya asiwe na udini wala ukabila na mzalendo wa nchi yake

Alisema kutokana na majina hayo ya urais pia katika tafiti zao imeonekana kuwa vyama vinavyoongoza katika kupendwa na wananchi ni pamoja na Chama cha Mapinduzi kuonekana kupendwa sana kuliko vyama vyote.

Alivitaja vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) 53.5,Chama cha Demokrasia (Chadema) 34.2 ,Chama cha Wazalendo (ACT)1.2 na Umoja wa Katiba Mpya (Ukawa) 6 na Chama cha wanachi CUF 6. 
Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Samunge Social Research Centre, George Nyaronga kutoka Chuo Kikuu Huria (OUT).
Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Samunge Social Research Centre, George Nyaronga (katikati), akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kuhusu viongozi wanaotaka kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu ambapo Waziri Mkuu wa zamani,  Edward Lowassa ameonesha kuwapiku wenzake kwa kupata asilimia 20 akifuatiwa na  Dk.Willibrod Slaa aliyepata asilimia 11.7. Kushoto ni Mtafiti Msaidizi wa utafiti huo, Wakili Mambo na kulia ni Mtafiti Msaidizi wa utafiti huo, Gideon Anyona kutoka Chuo Kikuu cha Kenyata.

Mkutano ukiendelea. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 27, 2015

    Aina hii ya utafiti unafaida gani kwa wananchi???Tena na waandishi wa habari wameitwa jamani Tz dah!!! na waandishi nao bize wanakopi mweee!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 27, 2015

    Dogo hacha njaa, yote hii ni njaa tu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 27, 2015

    Mnatoa utafiti bila ya kuonesha idadi kamili ya watu mliowafanyia hiyo research?!! Kutoka Maeneo gani?? Je wana umri gani?? je wamejiandikisha kupiga kura?? je wana kipato gani na elimu gani?? Huu utafiti una walakini kabisa na sitoweza kuuweka kichwani kabisaaa, eti siku moja baada ya kutangaza kugombea Urais na kuita waandishi leo hii kijana mwenye njaa na kujipendekeza kashafanya utafiti wake!!

    Jifunzeni toka kwa wenzenu www.gallup.com wanafanya tafiti za manufaa ya nchi zao SIO tafiti za kulipwa kisa una njaa na Umasikini wako. This is too cheap publicity!

    Hii Tanzania sijui tunaelekea wapi! We need to be very serious with our Country na msipoangalia mtakuja kushindwa baadae kutoa majibu ya maswali ya watoto wenu na Vizazi vijacho...

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 27, 2015

    Kama kweli CCM watamteua Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa rushwa kuwania urais, basi kujiuzulu hakuna maana kama alama ya uwajibikaji katika nchi hii ya Tanzania. Sasa kujiuzulu maana yake nini hasa??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...