Pazia la Tamasha la kwanza la Mavazi ya Heshima STARA limezinduliwa hivi "Stara Street Fashion"

Tamasha hili la aina yake linatazamiwa kufanyika tarehe  13th June 2015 katika ukumbi wa City Garden, kuanzia saa moja usiku hadi saa nne usiku kwa kiingilio cha shilling elfu 20 tu.

Pazia  la Tamasha hili litafunguliwa wiki moja kabla ya Tamasha kwa Exhibition ya bidhaa ya vitu mbalimbali... vitakavyouzwa kama vile Mabaibui, Udi Hena na vitu vingine kuanzia saa mbii asubuhi hadi saa 1usiku na hakuta kuwa na kiingilio, ni Buree

Tamasha hilo ambalo litafanyika kwa mara ya kwanza katika historia linatarajiwa kupambwa na Mavazi ya STARA. pamoja na mada mbalimbali kuhusu Nafasi ya Mwanamke katika Ndoa, Ujasriamali, Utunzaji wa Fedha na Mazungumzo kuhusu Mavazi ya Heshima sehemu za kazi. 

Akizungumzia kuhusu tamasha hilo Mratibu wa tamasha Latifah Makau Shekhoza alisema Wahudhuriaji watatakiwa kuwa wamejistiri na watoto wataruhusiwa.

Latifah Alisema ingawa Fashion show itahudhuriwa na wnawake pekee, exhibition itakuwa wazi wa watu wote.

Aliwataja wadhamini wa Tamasha hilo kuwa ni I-view Studio, Vayle Springs, AA Shekhozah co. Ltd, City Garden, Event Lights, Sofia Production, Gs1, Tanzania Women Bank, Clouds FM, Rehema Samo  na wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...