Balozi Dr Mahiga -Iringa mjini.

Na matukiodaimaBlog
ALIYEKUWA balozi wa kudumu  wa umoja  wa mataifa (UN) na mgombea urais katika mchakato  wa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) balozi Dr Augustono Mahiga anayeomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM amewashangaa makada  maarufu wa chama  hicho  walioshindwa katika mchakato wa ndani ya chama kwa nafasi ya urais kuhama chama hicho kuwa hao hawakuwa na mapenzi ya kuwatumikia  watanzania na kuwa watazunguka kote ila chama makini ni CCM pekee na kuwataka wana CCM jimbo la Iringa mjini kumpa nafasi yeye ili kuondoa masalia ya Chadema .

Balozi Dr Mahiga  alisema kuwa wana CCM hao  walioanza kuhama chama  kwa kukosa nafasi ya urais hawakuwa na mapenzi mema na CCM bali  walikuwa wawametanguliza  maslahi yao mbele na  kuacha kuangalia maslahi ya Taifa na chama hivyo ni vema watanzania  kuwatazama kwa jicho la tatu na ikiwezekana kuwachunguza japo kwa miaka 5 bila kuwachagua kuwa  viongozi  wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2015

    SASA DR MAHIGA UNAPINGANA NA MAELEZO AU USIA WA MWALIMU BABA WA TAIFA NA MUASISI WA CCM MAREHEMU MZEE JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALITUAMBIA IKIWA HATUTAPATA MAGEUZI NDANI YA CCM TUKAYATAFUTE NJE YA CCM NA CCM SIO BABA YETU WALA MAMA YETU SASA UNATU SHAURI TUBAKI KWA KUWA MAGEUZI UTAYALETA WEWE PEKE YAKO NDANI YA CHAMA CHETU?

    KUHAMA CHAMA CHA SIASA SIO AIBU UZOEFU WAKO NJE YA NCHI KAMA BALOZI UNALIJUA HILI SASA KWA NINI UNAANZA KUMWAGA MATOPE KWA WALE WANAO TAKA KUHAMA CHAMA HUO NI UAMUZI WAO NA NI HAKI YAO HATA KAMA CHAMA CHA CCM BADO KIKO MAKINI HAKATAZWI WALA ASILAUMIWE MTU KUCHAGUA KWA KWENDA VYAMA VINGI VINA MIIKO NA MILA ZAKE HUU NDIO UTAMADUNI WA MFUMO WENYEWE,TUOMBE KURA BILA KULAUMU UHURU WA WENGINE HUKO NI KUVUNJA MIIKO YA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI SISI CCM NI LAZIMA TUWE MFANO WA HAYA MABADILIKO TUKICHELEWA TUTAMALIZWA NA WENYE KUFUATA KANUNI NA UTARATIBU TULIO UCHAGUA.

    MDAU.
    MKEREKETWA.{IRINGA}

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...