Na woinde shizza.
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Filex Mabula amesema taarifa zilizotolewa kuwa halmashauri hiyo imetumiavibaya zaidi ya sh508.6 milioni fedha za shule na za kusambaza maji vijijini, zilizotolewa na benki ya dunia, siyo za kweli.

Akizungumza na waandisi wa habari jana, Mabula alisema halmashauri hiyo
ilitoa sh225.5 milioni kwenye shule za bweni kwa ajili ya chakula kwa mwaka 2013 hadi 2014 sawa na asilimi 281.9 ya fedha zilizoidhinishwa na hazina.

Fedha zetu zinatumika kwa kufuata kanuni na taratibu ndiyo sababu mkuu wamkoa wetu Joel Bendera alitupongeza Hanang’ kwa kupata hati safi kwa maraya nne mfululizo kupitia ukaguzi wa ripoti ya CAG,” alisema Mabula.

Alisema sh283.1 milioni zilipelekwa kwenye shule za Katesh, Balang’dalalu,
Bassodesh na Gendabi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya shule na kamati ya
fedha iliidhinisha kwa kikao cha Juni 26 mwaka huu na baraza la madiwani
Julai 8.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...