Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa nchini limemfungia msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zuena Mohamed kwa jina la kisanii Shilole kufanya shughuli za sanaa nchini kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 24/07/2015 hadi tarehe 24/07/2016.

Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 09/05/2015 akiwa katika onyesho lake la Muziki nchini Ubelgiji alikiuka maadili ya kazi ya sanaa mbele ya hadhira ya  wapenda sanaa za Tanzania na hivyo akadhalilisha utu wake na jamii ya Kitanzania kimaadili.  Pia itakumbukwa kwamba mnamo mwezi Oktoba, 2013 BASATA ilimuonya na akakiri kwa kuomba msamaha kwa tabia yake ya kucheza bila kuzingatia utu na maadili awapo jukwaani.

BASATA ilimpa nafasi ya kutoa maelezo yake kwa nini asichukuliwe hatua  za kinidhamu kwa kitendo chake cha kudhalilisha maadili, utu na sanaa ya Tanzania lakini akakaidi kutoa maelezo.  Hivyo basi BASATA imejiridhisha kwamba alikiuka maadili ya kazi ya sanaa  kwenye onesho lake la   huko Ubelgiji makusudi na amekiuka Sheria, Kanuni  na Taratibu za uendeshaji wa Sanaa. 

Hivyo basi kutokana na ukiukwaji huo wa sheria na kanuni za uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini, Baraza la Sanaa la Taifa chini ya Kanuni ya 30(1)(d) ya G.N 322 ya 2005 limemsimamisha kujishughulisha na kazi za Sanaa nchini kwa muda wa Mwaka Mmoja tokea tarehe 24/07/2015.  

Hivyo haruhusiwi kufanya au kushiriki kwa namna yoyote ile shughuli yoyote ya onesho la sanaa nchini au nje ya nchi. Iwapo atafanya kinyume cha hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi ikiwa ni pamoja na yeyote yule utakaye shirikiana naye.

Ni matumaini ya Baraza la Sanaa la Taifa kwamba wasanii na waandaaji wa shughuli za sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2015

    Show ilifanyika ulaya sio tanzania sasa basata kwa nini mumfungie msanii wetu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2015

    Who's shilole?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2015

    Akale wapi sasa jamani!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2015

    Tanzania utafikiri North Korea, udikteta sijui utakwisha lini. wabelgiji wenyewe hawajalalamika wala nini lakini madikteta wa Tanzania wanawaamulia wabelgiji.
    Kitu kikubwa kinachosumbua Tanzania ni umaskini wa fikra na kuchukiana waafrika kwa waafrika angekua mzungu wangemsifu tu. Unashangaa hata airport yetu Dar akija mzungu anahudumiwa haraka lakini ukisogea tu mtanzania kila mtu kakunja uso wala hujaliwi.

    ReplyDelete
  5. Safi sana anaharibu taswira ya jamii mambo yasirini anaweka hadharani

    ReplyDelete
  6. Taswira ya nchi inaharibikaje?? Ungesema taswira ya nchi inaharibiwa na ufisadi ningeelewa lakini kumfungia msanii ambaye hakufanya kosa la kudhuru mtu halafu hata show yenyewe haikuwa hapa nchini ni KUMUONEA. Sasa ataishije na hiyo ndiyo kazi mnamfungia? Naamini sasa nchi hii inaongozwa na viongozi wabovu kuliko wanaoongoza North Korea ambao hawatimizi wajibu wao lakini wanaongozwa na kufuatilia matukio tu.

    ReplyDelete
  7. HUU NI UONEVU WA DHAHIRI PAMOJA NA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINAADAMU< HIVI MNAPOMFUNGIA HUYU DADA ATAISHI VIPI ILHALI HII NDIO KAZI INAYOMUINGIZIA KIPATO?????

    ReplyDelete
  8. Sawa inawezekana ikawa ni sahihi kwa BASATA kusimamia kikamilifu sheria na taratibu zinazoendesha sanaa hapa TANZANIA na pia kuwasimamia wasanii husika wanapowakilisha TAIFA nje ya nchi.
    Uvunjaji wa taratibu zozote kikawaida unaenda na makaripio au aina nyingine ya adhabu yenye nia ya kuhakikisha kuwa kosa husika hariludiwi na pia kumfanya mhusika kujutia kosa alilofanya,Adhabu inaweza kugeuka kuwa kukomoa pale tunaposhindwa kuitoa kwa makusudio sahihi.Je Sheria za BASATA zinaelezea kiufasaha makosa yanayoweza kupelekea Msanii kupata adhabu ya namna hiyo?Je! sheria hizi zinaelezeaje pale kosa linapofanyika sehemu nyingine ambayo sehemu hiyo husika haina sheria inayotambua kitendo husika kama ni kosa?
    Je?Sheria za BASATA na wasimamizi wa Sheria husika wamekuwa vipofu kwa vitendo kama hivyo vinavyo fanywa na wasanii wengine wa ndani na nje ya nchi?
    Je utaratibu gani ulitumika kuamua kuwa adhabu iwe ni kufungiwa mwaka Mzima?Je haikuwa ni busara kuweza kumpa karipio kwa kosa la kwanza ambalo mhusika alishaomba msamaha?
    Tukigeukia kwenye uzito au ukubwa wa adhabu ,je ni sahihi kwa msanii ambaye sanaa yake ndio kazi yake kumpa adhabu ya kumfungia mwaka mzima kutokujihusisha kwa namna yoyote na sanaa yake?
    Ukubwa wa adhabu una mashaka makubwa na umebeba nia ya kuua sanaa ya mhusika!
    BASATA Itafakari adhabu yake ,iipunguze na kumpa fursa mhusika kujirekebisha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...