Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akiwasilisha taarifa ya

maandalizi ya sherehe za Nane Nane Kanda ya Kati zitakazo fanyika
sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Kitaifa kuanzia Agosti
Mosi Mkoani Dodoma.


Sherehe za Nane Nane Kanda ya Kati zitafanyika sanjari na Maonesho na mashindano maalum ya mifugo ya 5 Kitaifa  katika  uwanja wa Nzuguni Dodoma kuanzia tarehe 01/08 hadi 08/08/2015.



Sherehe za Nane Nane mwaka huu 2015 zinakwenda kwa Kaulimbiu inayosema “Matokeo Makubwa sasa  (BRN)– Tuchague viongozi bora kwa maendeleo ya Kilimo na Ufugaji” Kaulimbiu hii imekuja wakati muafaka ambapo Taifa letu la Tanzania linaelekea katika Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba na tayari baadhi ya vyama vya siasa vimeshaanza mchakato wa kuendesha kura za maoni ili kupata wagombea wa nafasi mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...