Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) imehitimisha rasmi Mradi wa Picture Afrika,tukio lililofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Mjini Njombe
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) Dkt Dugushilu Mafunda akizungumza wakati wa kutamatisha Mradi wa Picyure Afrika.Pamoja naye ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Dkt Rehema Nchimbi(wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mh Sara Dumba(wa kwanza kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Njombe Bw Noah Lameck

Poverty and Information and Communication Technologies for Urban and Rural East African Coutries(PICTURE AFRICA) ni Mradi ulifadhiliwa na Shirika la la Kimataifa la Maendeleo ya Utafiti la nchini CANADA (IDRC) ukihusisha nchi Nne za Afrika Mashariki zikiwemo Kenya,Rwanda,Tanzania na Uganda.Nchini Tanzania Mradi huo ulihusisha wajasiriamali wa Njombe na Makambako.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha Mradi huo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Dugushilu Mafunda amesema kuwa mwaka 2008 COSTECH ilitekeleza Mradi wa Miaka Mitatu wa Kuondoa Umaskini kwa wajasiriamali wa mijini na vijijini kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(PICTURE AFRICA).
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Dkt Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa kuhitimisha Mradi wa Picture Africa.Pamoja naye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mh Sara Dumba(wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) Dkt Dugushilu Mafunda(wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Njombe Bw Noah Lameck

Dkt Mafunda anasema kuwa COSTECH yenye jukumu la kuratibu na kuendeleza Tafiti nchini iliamua kusaidia utafiti huo ili kuhawilisha teknolojia ya habari na mawasiliano kwa wajasiriamali wa Njombe na Makambako lakini pia kuweza kuishauri serikali umuhimu wa kuboresha mazingira ya biashara za wajasiriamali wadogo na wa kati maeneo ya Njombe na Makambako.
Mtafiti Mkuu katika Mradi huo, Prof. Ophelia Mascarenhas anasema lengo la Mradi huo lilikuwa Kuondoa Umaskini mijini na vijijini kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Simu za Mikononi,Kompyuta na Mtandao wa Intaneti).

Prof. Ophelia Mascarenhas anaongeza kuwa utafiti huo umeweza kuonyesha kwa kiwango kikubwa ushahidi wa kisayansi wa uhusiano kati ya utumiaji wa TEHAMA na ukuaji wa uchumi kwa maeneo ya Mijini na Vijijini.
Picha ya Pamoja

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Dkt Rehema Nchimbi akihitimisha hafla ya kutamatisha Mradi huo,amesema Mradi huo umefanikiwa kuwapatia uwezo Wajasiriamali wa Njombe na Makambako kutokana na Sera nzuri za Serikali kutumia utafiti kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

“Wajasiriamali wengi wa Njombe na Makambako walipatiwa Simu,Kompyuta na Mtandao wa Intaneti ili kurahisisha biashara zao.”Anaeleza Dkt Nchimbi na kuongeza TEHAMA imerahisisha kupunguza gharama ya usafiri na biashara kwa kuwa inaifanya Dunia kuwa ndogo kama kijiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...