Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye hafla ya ufungaji wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la Envirocare ambapo Kongamano hilo limefanyika kwa siku tatu kuanzia Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungaji wa Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema akitoa neno la shukrani kwa Washiriki kabla ya kumkaribisha Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza kufunga Kongamano hilo.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akiwa ameongozana na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(kushoto) tayari kwa ufungaji rasmi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria ambalo limefanyika Mkoani Morogoro kuanzia Septemba 02 - 04, 2015(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...