Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa (pichani) amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.
Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, Mkwasa amesema vijana wake wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa Taifa Stars.
“Tumefanya mazoezi kwa takribani siku kumi, vijana wako katika hali nzuri ya mchezo, uwezo waanaouonyesha mazoezini ni wa hali ya juu na unatupa matumaini ya kufanya vizuri” Alisema Mkwasa.
Aidha Mkwasa amesema katika mpira hakuna kinachoshindakana, anatambua Nigeria ni timu kubwa Afrika, wameshatwaa ubingwa wa Afrika mara tatu, lakini mpira wa sasa lolote linaweza kutokea, hivyo sisi tumejiandaa vilivyo kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mwisho Mkwasa amesema wamejindaa vizuri kwa mchezo huo wa kesho, na kuwaomba watanzania kuja kuwapa sapoti wachezaji uwanjani kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo, na kusema kikosi chake hakina mchezaji majeruhi hata mmoja kuelekea kwa mechi hiyo.
Mechi hiyo ya kesho jumamosi itachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Rwanda ambao ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore Simba (mwamuzi msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), Abdoul Karim Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) na kamisaaa wa mchezo ni Charles Kasembe kutoka nchini Uganda ambao wote tayari wameshawaili jijini Dar es salaam tangu jana jioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...