Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni ukipenda waiite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien's yenye makao kule Ujerumani inatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Vechelde Festival nchini Ujerumani leo kuanzia saa 2:00 Usiku katika eneo la Bürgerzentrum Vechelde liliopo mtaa wa Hildesheimer Straße 5 mjini Vechelde jirani mji wa Braunschweig
Bendi hiyo maarufu Ngoma Africa yenye sifa za kuwatia kiwewe washabiki wa muzikikatika maonyesho ya kimataifa kwa kutumia mdundo wao "Bongo Dansi" made in Uswahilini ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyoweza kudumu kwa miaka 22 na kufanikiwa kukama soko la kutumbuiza katika maonyesho ya kimataifa. 
Kwa sasa bendi hiyo inatamba na CD yake mpya ya "LA MGAMBO" yenye nyimbo mbili za kumuaga rais Jakaya Kikwete na CD hiyo utunzi wake Kiongozi wa bendi Ebrahim makunja aka Kamanda Ras Makunja imeshatua nchini Tanzania tayari kwa kutingisha anga katika vituo vya redio mbali mbali.
wasikilize ffu-ughaibuni at www.reverbnation.com/ngomaafricaband

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...