Watanzania wanaoishi ughaibuni (diaspora) wametakiwa kuwa kichocheo cha kuleta maendeleo ya biashara na uwekezaji katika nchi yao ili kuongeza pato la taifa na kuboresha maisha ya mwananchi wa kawaida. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakati wa kufungua kongamano la wafanyabiashara linalofanyika Birmingham, Uingereza tarehe 4 na 5 Septemba 2015. Aliwaasa washiriki wa kongamano hilo kulitumia kama jukwaa la kufanya majadiliano kwa madhumuni ya kubadilishana mawazo mapya ili kuibua fursa lukuki za uwekezaji nchini Tanzania. Aidha, aliwahimiza wanadiaspora kushirikiana na wajasiliamali wa nyumbani ili kuzitumia fursa hizo ipasavyo.

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe
Balozi Mulamula aliwahakikishia wnadiaspora waliohudhuria kongamano hilo, kuwa Serikali ina dhamira ya dhati ya kuwashirikisha Watanzania wanaoishi ughaibuni ili kuchangia maendeleo ya nchi yao. Hivyo, aliwahimiza kuja kuwekeza nyumbani kwa kuwa Serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwapatia ardhi kwa ajili ya kujenga makazi au kuwekeza.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tujifunze katika nchi zilizoisha piga hatua ya kuwezesha wanadiaspora wenye uwezo wa kuwezeshwa kupata mikopo mikubwa au kuleta fedha zao kutoka nje kuwekeza nyumbani nusu nusu na wawekezaji wa nje.

    Uwezekano wa kuwa na Bond zinazotegemea uwekezaji wa wana diaspora wenye uwezo wa kifedha kuchangia miradi ya nyumbani ili kupata faida ni njia zinazoweza kuangaliwa uwezekano wake nchini kama njia mbadala za kuwezesha diaspora kupata faida wakati tunaongeza mapato zaidi ikiwemo fedha za kigeni nchini.

    Tunawezesha kujifunza kutokana na nchi za kiafrika zilizojaribu njia hizi mbili kabla hatujazitumia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...