Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk.Fatma Mrisho (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka 2015 yatakayofanyika kitaifa Desemba Mosi mkoani Singida. Kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi.


Na Dotto Mwaibale
 
MAAMBUKIZI ya virusi vya Ukimwi nchini yameongezeka kwenye kundi la vijana wenye umri wa miaka kati ya 19 mpaka 24 tofauti na ilivyokuwa miaka minne iliyopita, ambako kundi lililokuwa limeathiriwa zaidi lilikuwa miaka kati ya 25 mpaka 34, imeelezwa.

Pia licha ya kwamba kiwango cha maambukizi mapya ya virusi hivyo nchini kimeshuka kutoka asilimia 7 mwaka 2004 mpaka kufikia asilimia 5.3 mwaka huu, takwimu za baadhi ya mikoa ikiwemo Singida, Kigoma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro na Kagera zimeonekana kuongezeka.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani kwa mwaka huu, Dk. Fatma Mrisho, alisema kazi kwa ujumla kazi kubwa imefanyika.
Ofisa Mipango wa Taifa wa UNAIDS, Fredrick Macha (kulia), akizungumza katika mkutano huo.


Alisema ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita, maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi yamepungua kwenye maeneo mengi ya nchi kutokana na jitihada za serikali, wadau na wananchi kwa ujumla.

Dk. Mrisho alisema licha ya mikoa kadhaa kuendelea kuandamwa na maambukizi hayo, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maendeleo na mwingiliano wa watu, mikoa ya Tanga na Manyara ndiyo yenye takwimu chache za maambukizi zikiwa na asilimia 4 pekee.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...