Na Binagi Media
Kwetu ni Wimbo unaofanya vizuri nchini na hata nje ya nchini ambapo kwa mara ya kwanza uliimbwa na Msanii Raymond kutoka WCB Wasafi. Kutokana na wimbo huo kuwa na mashairi mazuri pamoja na melodi yenye kuvutia, Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza ameurudia wimbo huo na kuuongezea ladha ambayo inaufanya kuwa wimbo bora uliorudiwa kwa sasa nchini. 
 "Nimeamua kuurudia wimbo huu kwa sababu umebeba ujumbe mzito ambao ulinigusa na kuamua kuurudia kwa njia zangu za pekee ili watanzania wayasikie maneno vizuri pasipo na shaka". Elizayo HB ameiambia BMG. Hakika Elizayo HB ameutendea haki wimbo huo ambayo umerekodiwa katika Studio za Brother's Music Jijini Mwanza, kwa ushirikiano wa producers Adof pamoja na Doncha Master.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...