Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. James Mataragio (mbele) akielezea mikakati ya shirika hilo katika matumizi ya gesi asilia inayozalishwa kwa ajili ya matumizi ya majumbani na nyingine kuuzwa katika soko la nje katika kikao kilichokutanisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya nishati, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili matumizi ya gesi iliyogunduliwa nchini katika matumizi ya ndani na nyingine kuuzwa nje ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2016

    Gesi hii imesambazwa mikoani pia mara ya mwisho nilipoenda likizo na kuiona wilayani nilinunulia jamii ya kijijini kwangu mtungi kampuni hiyo iliniambia mtungi ukiisha wambie wapige simu tutawauzia gesi haya ni maendeleo mazuri. Ujumbe watanzania tuinue wengine ili waboreshe kipato na hali ya maisha ikiwemo makazi ili waweze kumudu hizi bidhaa na huduma za gesi, watumie umeme, wahifadhi maji hata ya mvua kwenye matanki makubwa ya maji. Kinachozuia ni uwezo duni wa wengi wanaohitaji kuinuka hata kama ni kwa kuwekeza kwenye maendeleo yao ili waweze kunufaika na kuchangia maendeleo vizuri zaidi kama wateja wa huduma hizi za karne hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...