Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Be.Sabasaba Moshingi,(kushoto), akijibu baadhi ya hoja za wajumbe wa Mkutano wa mwaka wa wanahisa wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam  Mei 25, 2016. 
Wajumbe walipokea taarifa ya uendeshaji Benki hiyo kwa mwaka 2015 ikiwa ni pamoja na mipango ya uendeshaji wa Benki kwa mwaka huu wa 2016. 
Pamoja na mambo mengine, Bw.Moshingi alisema benki inampango wa kuingia kwenye soko la his a(Dar es salaam stock exchange), sambamba na kuongeza Huduma za ATM kwenye matawi yake mbalimbali kote nchini. Katikati no Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Lettice Rutashobya, na kulia in Katibu wa Bodi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Benki hiyo, Bi.Mystica Mapunda Ngongi.
Wakichangia hoja mbalimbali baada ya kupokea taarifa ya mahesabu ya fedha iliyosomwa na Meneja wa kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Nexia SJ Tanzania, Bw.Fulgensio Mgaya, ambaye alisema mahesabu ya Benki hiyo hayakukutwa na dosari, wajumbe wa mkutano huo, Bi.Theresia A Chitumbi na Bw. James Sando, wameupongeza uongozi wa Benki hiyo kwa usimamizi thabiti na uendeshaji mzuri wa Benki. (PICHA NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettice Rutashobya, (wapili kulia), akiendesha mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam Mei 25, 2016. Kikao hicho kimejadili utendaji kazi wa benki katika mwaka wa 2015/2016 ambapo wajumbe walijadili mapato ya benki, upanuzi wa huduma za kibenki nchini ikiwa ni pamoja na mabporesho ya huduma kwa wateja. Wengine pichani kutoka kulia, ni Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Bw. Hamisi Mussa Omar. 
 Wakurugenzi wa idara mbalimbali za TPB, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...