Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Obrey Chirwa akiichambua ngome ya timu ya TP Mazembe, katika mtanange uliopigwa jioni hii kwenye dimba la Taifa (Uwanja wa Taifa) Jijini Dar es salaam, ikiwa ni Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Hadi kupanga cha mwisho kinalia, Yanga wamelala kwa bao 1-0.
Mshambuliaji wa Timu ya TP Mazembe, Mtanzania Thomas Ulimwengu akichuana vikali na Beki wa Yanga, Kelvin Yondani, katika Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, uliopigwa jioni hii kwenye Uwanja wa TAifa jijini Dar es salaam. Yanga imelala kwa bao 1-0.
Beki wa TP Mazembe, Christian Nekadio akiruka juu kuondosha hatari iliyoelekezwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Yanga, Juma Hassan Mahadhi.
Kipa wa Yanga,Deogratius Munish 'dida' akinyaka mpira kwa umaridadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...