Benki ya Advans ya Tanzania
imebadili jina kuwa Letshego Bank (T) Limited kufuatia umiliki wa asilimia 75
za hisa za benki hiyo iliyonunuliwa na kampuni ya Letshego Holdings Limited
baada ya kuwekeza zaidi ya Shilingi bilioni 19.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa muonekano
mpya wa benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw. Yohane Kaduma alisema umiliki huu uliyofanyika tangu mwaka 2015, umefanya Letshego
kuwa mbia mkuu wa benki hiyo huku asilimia 25 ikiendelewa kumilikiwa na
wanahisa waanzilishi ambao ni Advans SA, na Shirika la Maendeleo ya Uholanzi
(FMO) ambao kwa mujibu wa Bw. Kaduma, watendelea kutoa ushirikiano kiuongozi na
kiutawala.
Bw. Kaduma aliongeza kuwa pamoja na kuzindua muonekano mpya
wa benki hiyo, Letshego ya Tanzania pia imezindua safari ya mabadiliko
itakayoiwezesha kuwa kinara katika kuvumbua na
kutoa huduma za kifedha ambazo ni shirikishi kwa wanajamii wote (financial
inclusion).Alisema uboreshwaji wa huduma zitakazotolewa na benki hiyo inalenga
kusaidia katika kutatua matatizo muhimu ya wateja wao ambayo ni pamoja na
kuweka amana, kukopa, kufanya malipo na hata huduma za bima.
“Mwonekano huu mpya wa Letshego Bank
ni badiliko ambalo linafanyika katika nchi zote 10 barani Afrika ambapo tupo, na
unazindua upya safari ya mabadiliko inayochukuliwa na Letshego. Kwa Tanzania,
mabadiloko tuliyoyafanya kama benki, yanaendana
pia na dira ya Serikali ya kuleta mendeleo ya kiuchumi na huduma za jamii kwa
wananchi wake,” alisema Bw. Kaduma.
Aliongeza kuwa benki ya Letshego inashauku ya kujenga
utamaduni chanya wa kukopa na ujumuishwaji wa kifedha kwa watanzania.“Tunafanya kazi ili kusaidia kuhakikisha kwamba huduma zetu
za kifedha zinaleta maana na mabadiliko kwa Watanzania. Wateja wetu ndiyo
wamewezesha jina na huduma zetu kukua kufikia hatua tuliyo nayo leo. Tunawashukuru
na tunawahakikishia kwamba tunafurahia kuendelea kutoa ufumbuzi wa kifedha
utakao boresha maisha yao,” aliongeza Bw. Kaduma.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kuboresha huduma zeo
ndani ya mwonekano huu mpya, pia benki hiyo itaendelea kufanikisha lengo lao la
kutoa huduma jumuishi za kifedha ambazo zitaleta uboreshaji wa maisha ya wadau
weo wote.
“Letshego Bank inaanzisha ufumbuzi wenye lengo la upatikanaji wa mikopo ya kilimo, elimu, afya na nyumba kwa
watu wenye kipato cha chini, cha kati na wajasiriamali wadogo. Wateja na wadau
wetu wote, wataendelea kupata huduma za kuweka akiba na kufanya malipo. Katika
hili, na ili kuhakikisha kwamba huduma zetu zinapatikana maeneo mengi ya
Tanzania, Letshego Bank ina mpango wa kutoa huduma za kibenki kupitia vituo
zaidi ya 100, kwa kuitumia Faidika kama wakala wake. Tunaamini kwa ushirikiano
wa vyombo husika, hili litawezekana, na Watanzania wengi zaidi watafurahia
huduma zetu,” alisema Bw. Kaduma.
Bw. Kaduma alifafanua kuwa hapa Tanzania, Letshego
imekuwako kwa miaka 10 sasa kupitia kampuni inayojulikana kwa jina la
kibiashara la Faidika.Aliongeza kuwa Advans
Bank (ambayo sasa ni Letshego Bank) imekuwako Tanzania kuanzia mwaka 2011. “Katika
miaka hii sita ya utoaji wa huduma za kifedha ambapo tumekuwako katika
mikoa ya Dar es Salaam (matawi 3), Mwanza na Mbeya, tumetoa ufumbuzi wa masuala
ya kifedha ambayo ni rahisi, stahiki, na nafuu kwa zaidi ya watanzania 26,000
nchi nzima,. Huduma hii ikitolewa na wafanyakazi zaidi ya 200 kwenye matawi
haya,” alifafanua Bw. Kaduma.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Letshego ni neno la ki-Setswana linalomaanisha ‘support’ – au
Harambee kwa Kiswahili, neno hili huashiria uwezo wa taasisi kuweza kushirikiana na serikali na watumishi
wa serikali, pamoja na wajasiriamali wadogo na wa kati (MSEs) ili kuweza kutoa huduma rahisi, nafuu na mahsusi zitakazoweza
kuboresha hali ya jamii.
“Muonekano wetu mpya ni wa kisasa zaidi na ukiendana na dhana nzima ya
‘Harambee’, inaonyesha msingi imara, na kwamba sote tunaweza kukua pamoja,”
alisema Bw. Kaduma.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Letshego ya Tanzania Bw. Yohane Kaduma (wa pili kulia) akionyesha nembo na muonekano mpya ya benki hiyo iliyobadilishwa kutoka kutambulika kama Advans Bank kuwa rasmi Letshego Bank. Wanaoshuhudia ni Dru Jayaratne (wa kwanza kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa FAIDIKA Bw. Mbuso Dlamini (wa pili kushoto) na Meneja Rasilimali watu wa benki ya Letshego Bi. Rehema Ngusar.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Letshego ya Tanzania Bw. Yohane Kaduma akiomwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa FAIDIKA Bw. Mbuso nembo na muonekano mpya ya benki hiyo iliyobadilishwa kutoka kutambulika kama Advans Bank kuwa rasmi Letshego Bank.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Letshego ya Tanzania Bw. Yohane Kaduma (wa pili kulia) akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa FAIDIKA Bw. Mbuso Dlamini (wa pili kushoto) mara baada ya kuzindua nembo na muonekano mpya ya benki hiyo iliyobadilishwa kutoka kutambulika kama Advans Bank kuwa rasmi Letshego Bank. Wanaoshuhudia ni Dru Jayaratne (wa kwanza kulia), na Meneja Rasilimali watu wa benki ya Letshego Bi. Rehema Ngusar.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...