Kampuni ya simu za mikononi Airel Tanzania leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu zikaoshiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ngazi ya mkoa ambayo inatarajiwa kuanza Julai 30 mpaka Agosti 30 2016 kwenye mikoa tofauti hapa nchini.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 200 vimekabidhiwa kwa Wasimamizi wa vituo vyote vya mikoa na Taifa. Vifaa hivyo hivyo ni pamoja na jezi za wachezaji, shin guards, soksi, jezi za marefa, mipira pamoja na glovu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Katimu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Celestine Mwesingwa alisema ‘ Kwa kutoa vifaa hivi vya michezo,mdhamini ametimiza moja kati ya majukumu yake na ni matarajio yangu kwamba mtarudi kwenye vituo vyenu na kuongeza bidii ya kutafuta vipaji vinavyoibuka vya mpira wa miguu’.

‘Tunatarajia kuona mechi zenye ushindani na za kuvutia na natoa wito kwa viongozi wa vyama vya mikoa kuwa makini wakati wa kuchangua timu kombaini ambazo zitakuja kucheza kwenye fainali za taifa ambazo zitafanyika Dar es Salaam tarehe 6 mpaka 11 Septemba mwaka huu.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema ‘Airtel Rising Stars inaungana pamoja na promosheni yetu ya Airtel Fursa ambayo ilizinduliwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao. Kwa mwaka, michuano hii inatoa fursa nyingine kwa wavulana pamoja na wasichana kutambua uwezo wao wa kucheza soka na kuweza kufanikisha ndoto zao. Kwa mantiki hiyo, Airtel Tanzania inatumia program hii kuwezesha vijana wenye vipaji vya mpira wa miguu kuvionyesha kwa makocha na hatimaye kufakinisha ndoto zao’.

Airtel Rising Stars ni mpango kabambambe kwa Afrika nzima yenye lengo ya kutoa nafasi kwa vijana kuonyesha vipaji vyao mbele ya makocha, na hatimaye kupata fursa ya kuviendeleza na kuvikuza.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.
Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu wa chama cha soka cha Ilala Daud Kanuti tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.
Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu wa chama cha soka cha Kinondoni Isack Mazwile tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...