Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.
Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria.
"Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa.
"Wananchi hawa wana shida. Na siasa nzuri ni wananchi washibe. Siasa nzuri ni wananchi wetu wapate dawa" amesema Rais Magufuli.

Kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali yake ya awamu ya tano tangu aingie madarakani Rais Magufuli ametaja baadhi ya hatua hizo kuwa ni kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zaidi ya laki moja na kuongeza fedha za miradi ya maendeleo katika bajeti ya serikali kutoka asilimia 26 ya mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia 40 katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017.

Hatua nyingine ni kuondoa wafanyakazi hewa 12,500 katika orodha ya waliokuwa wanalipwa mshahara na serikali, kudhibiti upotevu wa mapato serikalini, kutenga shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard gauge na pia akazungumzia hatua zilizochukuliwa dhidi ya wala rushwa na wanaojihusisha na ufisadi kwa kuunda mahakama ya mafisadi huku akiapa kuwa katika kipindi chake hakuna fisadi atakayeendelea kutamba.

Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Ikungi na baadaye amefanya mkutano wa hadhara Singida Mjini ambako amesisitiza kuwa serikali yake haiko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ahadi na Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Singida

29 Julai, 2016


Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Manyoni Mkoani Singida mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Singida.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia wakazi wa Singida mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wakazi wa Manyoni mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
Mbunge wa manyoni Magharibi Yahya Masare akicheza ngoma na kikundi cha Ngoma za asili cha Manyoni kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli kuhutubia mkutano katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tambuka Reli Manyoni Mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Ikungi waliomsimamisha wakati akielekea Mkoani Singida. PICHA NA IKULU 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2016

    The President is absolutely correct. Chaos under the pretext of democracy shud never be tolerated. The can call him what they desire - as long as he is attending to the bread and butter issues of our people he wud have our backing. God bless Magufuli and God bless Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2016

    Sema Rais sema! Hao wapinzani wanataka kujaza mifuko yao tu, mengine wongo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2016

    Ajenda hapa ni kuboresha na kujenga shule, kujenga barabara na miundombinu, kuboresha huduma za afya, kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuimarisha masoko. Wapinzani wasituvuruge. Demokrasisa waanze kuonyesha kwenye vyama vyao viwe vya kitaifa sio kikanda!

    ReplyDelete
  4. Over the years Tanzania has been unable to make sustainable economic growth even though we are blessed with vast amount of wealth. Majority of people have been suffering as a result. But under the stewardship of President JP Magufuli, Tanzanian are feeling blessed. So people let's all unite,work hard and support our beloved President.
    Don't waste your time demonstrating for nothing. God bless TZ.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2016

    Tatizo kuna wanasiasa wanataka kuwatumia wananchi kama mtaji wao wa siasa chafu. Kwanini msiweke focus ya maendeleo kwenye maeneo mloshinda uchaguzi kuliko kuliko kuwapotosha wananchi wenye kiu ya maendeleo. Hapa kazi tu, usanii wenu mbele ya namanga uko, aala!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...