Mhariri Mkuu wa kituo cha redio cha EFM Radio cha Jijini Dar es Salaam, Scholastica Mazula akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za redio hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi. Kulia ni Mtangazaji wa redio hiyo, Boneventure Kilosa.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha michezo cha redio ya EFM, Ibrahim Masoud “Maestro” wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni kinachorushwa hewani na kituo cha redio ya EFM, Silvester Mjuni (kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi. Wengine kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Jonas Kamaleki na Afisa Habari Beatrice Lyimo.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akizungumza katika mahojiano maalum ya kipindi cha cha UBAONI kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha EFM redio cha Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Jonas Kamaleki.(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA -MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...