Na Georgina Misama – MAELEZO.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limejipanga kumaliza kero ya makazi ya nyumba kwa watanzania ifikapo mwaka 2025, kwa mujibu wa Meneja Mauzo wa Shirika hilo,  Bw. Erasto Chilambo. Kasema hayo  wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Bw. Chilambo alibainisha kuwa nyumba zisizopungua elfu 30 zitajengwa kwa ajili ya kuuzwa na kupangishwa ambapo katika nyumba hizo watu wa kipato cha chini, kati na juu ndio walengwa.
“Katika mkakati huu, Shirika limekusudia kujenga nyumba 12000 kwa ajili ya watu wa kipato cha chini, nyumba 13500 kwa ajili ya watu wenye kipato cha kati na nyumba 2700 kwa ajili ya watu wenye kipato cha juu.” Alisema Chilambo, akiongezeakuwa Shirika linajenga majengo 1800 ya kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini, ambayo yanatazamiwa kukamilika ifikapo 2025.
“Katika kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma, shirika linajenga nyumba za makazi 300 zitakazouzwa kwa watumishi wa Serikali, ambazo zina ukubwa tofauti zenye vyumba 3 kila moja.” Alisema Bw.Charahani.
Tangu kuanzishwa kwake Shirik la Nyumba limekuwa likimiliki na kuuza majengo mbalimbali. Hivi sasa shirika linamiliki MAJENGO 2483 yenye sehemu 18121 za makazi na biashara katika Mikoa ya Tanzania Bara.
Meneja Mauzo wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Bw. Erasto Chilambo akizungumza na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mkakati wa shirika hilo kujenga nyumba 300 zitakazouzwa kwa watumishi wa umma Mkoani Dodoma ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa makazi kwa watumishi wanaohamia Mkoani humo na kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamia mkoani humo.kushoto ni Afisa Habari wa Shirika hilo Bi Edith Nguruwe.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa NHC leo Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...