Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo amezindua Mafunzo ya  namna ya Kutengeneneza Taa na Chaja zinazotumia mwanga wa jua kwa vijana 20  katika Kata ya Nyegina Mkoa wa Mara.

Akifungua mafuzo hayo Profesa Muhongo amewataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri wakati wanapohudhuria mafunzo na kueleza kuwa, yatakuwa chachu katika kupanua wigo wa  wa ajira ikiwemo wahitimu kujiari wenyewe.

Profesa Muhongo amewataka vijana na wananchi mkoani humo kuweka nguvu kubwa katika elimu kutokana na umuhimu  na mchango wake kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akizungumzia kuhusu Mradi wa Usambazaji Vijijini Awamu ya Tatu, Profesa Muhongo ameeleza kuwa, awamu hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa, mradi huo utafanywa kwa Awamu na kusisitisza kuwa, adhma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, ndani ya kipindi cha miaka mitano vijiji vyote nchini viwe vimeunganishwa na nishati hiyo.

" Vijiji vyote vitaunganishwa na nishati ya umeme. Tutasambaza  awamu kwa awamu na lengo letu ni kuhakikisha kuwa, vijiji vyote chini vinaunganishwa na umeme ndani ya kipindi cha miaka mitano. Wale ambao hawajafikiwa awamu ya kwanza na ya pili tutawafikia awamu ya tatu vivyo hivyo mpaka tufikie lengo letu," amesisitiza Prof. Muhongo.

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung ambaye nchi yake imefadhili mafunzo hayo, amesema kuwa,  uwepo wa taa hizo utasaidia upungufu wa umeme hususan maeneo ya vijijini na ambayo bado hayajaunganishwa na nishati hiyo.
Aidha, amesema kuwa, mafunzo hayo ni fursa ya ajira kwa wahitimu watakaopata mafunzo hayo ikiwemo nafasi za kuajiriwa na hivyo kuwataka kutilia mkazo mafunzo hayo na kueleza kuwa, mafunzo hayo ni mwanga kwa vijana.

Aidha, ameongeza kuwa,  kutokana na urafiki wa miaka mingi baina ya nchi za Tanzania nasini , hirikinchi hiyo itlea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na umeme wa uhakika.
"Kama ilivyo kwa kaulimbi ya Awamu ya  Tano ya Rais Dkt. John Magufuli, Hapa Kazi Tu' na mimi napenda kusema tusiende polepole twende 'Haraka, Haraka", amesisitiza Balozi  Geumyoung.
Kwa mujibu wa Professa Muhongo mafunzo hayo yanatarajiwa pia kutolewa katika  Kata za Mwirangi, Bukima na Mgango.

 Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dkt.  Hong- Kyu Choi, amesema kuwa, baada ya kuzifikia Kata zote zilizoainishwa, watachaguliwa wanafunzi bora ambao watakuwa mabalozi wa mafunzo hayo na hivyo kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kufuatilia mafunzo hayo na kuyachukulia kwa uzito mkubwa.

Mbali na kufungua mafunzo hayo, Profesa Muhongo pia amekagua miradi ya umeme Awamu ya Pili inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kome katika kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi.
Mafunzo hayo yamezinduliwa tarehe 20 Februari,2017
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akionesha mfano wa Taa zinazotumia mionzi ya jua ambazo vijana 20 katika Kata ya Nyegina watafundishwa namna ya kuzitengeneza baada ya kuzindua mafunzo hayo. Kulia ni Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi.
Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza Taa na Chaja zinazotumia mionzi ya jua, Dkt. Dkt. Hong- Kyu Choi, akiwaleza washiriki wa mafunzo namna mafunzo hayo yatakavyoendeshwa.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Dkt. Vicent Naano, (wa tatu kushoto) akiongea jambo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo ya Kutengeneza taa na chaja zinazotumia mionzi ya jua. Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muongo (katikati), Balozi wa Korea Kusini nchini,Song Geumyoung Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi (wa pili kulia) na baadhi ya wawakilishi wa vijana wanaoshiriki mafunzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...