Picha zote na Fredy Njeje

"Kiongozi bora ni pamoja na yule ambaye anahakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na watu anaowaongoza" hayo yalisemwa na bwana Nelson aliyekuwa mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Nchini Tanzania wakati wa semina ya vijana katika kushiriki programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Global Peace Foundation Tanzania. 

Alisema kuwa kiongozi makini ni yule anayehakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na kuwafanya wafanyakazi wake waishi kama familia moja ili kuondoa migogoro mbalimbali ambayo inaweza ikazuirika.

"Amani inatakiwa kudumishwa kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla" alisema Nelson na kuongeza kukosekana kwa amani kunaweza kusababisha maafa kama vifo kwa sababu ya vita pia uchumi kuyumba kutokana na watu kuhofia kufanya shughuli za kimaendeleo kwa sababu ya machafuko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa uelewa ili wapate kujiunga.

Nae Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili ‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.
Muandaaji wa Semina hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Vijana kutoka Maeneo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yanazungumziwa wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Kigamboni .
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Bw. Nelson akieleza namna viongozi katika sekta mbalimbali wanavyoweza kusaidia kudumisha amani katika Jamii.
Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi Bw. Anthony Luvanda akitoa masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...