Na HAMZA TEMBA - WMU.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne
Maghembe ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia
Hifadhi ya Taifa ya Arusha kuhakikisha kuwa wananchi wote waliolima ndani ya
eneo la hifadhi hiyo kinyume cha sheria wanaondoa mazao yao pamoja na kusitisha
kabisa shughuli zozote za kibinadamu ndani ya hifadhi hiyo.
Prof. Maghembe ametoa agizo hilo jana wakati akiwa
kwenye ziara yake ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo iliyopo wilaya ya
Arumeru mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na
hifadhi hiyo ikiwemo maeneo yenye mgogoro kwa ajili ya kuyatafutia ufumbuzi.
"Naagiza, kuanzia leo ni marufuku mtu yeyote
kuonekana akilima katika eneo hili, wekeni askari hapa, atakayeonekana piga
pingu, hatuwezi kushuhudia watu wanalima ndani ya hifadhi tukae kimya, ni
lazima tuchukue hatua. Watangaziwe na wapewe muda wa kuondoa mazao yao, ndani
ya siku 30 au 40 wawe wameshaondoka", alisisitiza Prof. Maghembe baada ya
kukagua eneo hilo.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akiingia
kwenye ofisi kuu ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha jana Mkoani Arusha katika ziara
yake ya kikazi ya siku moja katika hifadhi hiyo iliyolenga kukagua shughuli za
uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi. Kushoto
kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Alan Kijazi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) na wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia taarifa kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Arusha ambayo iliwasilishwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Steria Ndaga.
Baadhi ya wanyamapori (Twiga na Pundamilia) wakionekana wakijivinjari ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Arusha wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe katika hifadhi hiyo jana ambayo ililenga kukagua shughuli za uhifadhi hususan maeneo yenye migogoro kwa ajili ya kuitafutia ufumbuzi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...