Ni baada ya TRA kuchunguza Kanisa Full Gospel Bible fellowship

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) uchunguzi ambao wameufanya kwenye Kanisa la Askofu wa Kanisa Full Gospel Bible fellowship, Zakaria Kakobe wamebaini kuwa kanisa hilo linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na majaba.

Wamesema kitendo hicho ni kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha lakini pia uwekaji na utoaji wa fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika huku ikibainika pia amekuwa mkwepaji wa kodi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema baada ya kufanya uchunguzi wamebaini mbali ya kuwa anatunza fedha nyingi kwenye ndoo na majaba , pia wamebaini hana akaunti yeyote nchini katika benki isipokuwa ni msimamizi wa akaunti ya Kanisa yenye fedha zaidi ya sh.bilioni nane.
Amesema katika uchunguzi huo wamebaini kuwa Kanisa limekwepa kodi ya zaidi ya Sh.bilioni 20 lakini amelipa baada ya kufanyika kwa uchunguzi huo wa TRA.
Pia uchunguzi wa TRA umebaini kuna kampuni ya watoto wa Askofu Kakobe kukwepa kodi ya zaidi ya Sh.milioni 37 ambazo ziliweza kulipwa na watoto hao.“Utaratibu wa utunzaji wa fedha za Kanisa kwenye ndoo na majaba ni kinyume cha utaratibu wa utunzaji fedha.Pia utoaji wa fedha nyingi katika akaunti haushirikishi vyombo vya ulinzi kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika,”amesema Kichere
Hata hivyo, amesema safari za nje za  Askofu huyo zinahusisha yeye na mkewe tu na kuhoji kwanini wengine hawasafiri katika safari hizo.Ikiwa pamoja na Kanisa hilo kushindwa kutengeneza hesabu za mapato na matumizi ya fedha jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya katiba na usimamizi wa fedha.
Ameeleza kwenye uchunguzi wa TRA umebaini kwamba fedha za Kanisa ndizo ambazo zimetumika kujenga nyumba ya mkewe Askofu Kakobe kwa jina lake kinyume na taratibu za Kanisa.
“TRA inatoa mwito kwa taasisi za dini nchini ambazo zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za kod.Pia taasisi za dini zifuate katiba zao pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumiz,”amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...